Ayatollah Ali Khamenei azidiwa na huzuni akimuaga Ebrahim Raisi

0:00

HABARI KUU

Kiongozi wa juu nchini Iran Ayatollah Ali Khamenei ameonekana kuzidiwa na huzuni na kuamua kuondoka baada ya kuongoza ibada ya sala ya kuaga miili ya aliyekuwa Rais wa taifa hilo Ebrahim Raisi na maafisa wengine waliokufa kwenye ajali ya helikopta, zoezi lililoshuhudiwa na maafisa wa ngazi za juu zaidi ya 40 kutoka mataifa ya kigeni mjini Tehran.

Khamenei ameongoza shughuli hiyo iliyofanyika katika Chuo Kikuu cha Tehran, ambapo vilio vilisikika kutoka kwa waombolezaji waliokusanyika kwa ajili ya kuwaaga viongozi wao, wakati majeneza yao yaliyokuwa yamezungushiwa bendera ya Iran, yalipopangwa mbele ya maafisa wandamizi.

Khamenei aliongozwa ibada hiyo akitumia kitabu kitakatifu cha Kiislamu cha Quran na aliondoka mara baada ya sala ambapo wakati wote Rais wa mpito wa Iran, Mohammad Mokhber alikuwa amesimama karibu na Khamenei akionekana kububujikwa na machozi.

Miongoni mwa waliohudhuria ibada hiyo ni pamoja na Maafisa waandamizi wa Kikosi cha Walinzi wa Kimapinduzi, chenye ushawishi mkubwa nchini humo, akiwemo Kiongozi wa Wanamgambo wa Hamas wa Palestina, Ismail Haniyeh.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Mfahamu Didi-Stone mmoja wa watoto 7 wa...
NYOTA WETU Didi-Stone Olomidé ambaye amepewa jina kutokana na mjomba...
Read more
Dkt Charles Kimei ahofia nafasi yake ya...
HABARI KUU "Mnataka nisirudi Bungeni?" Mbunge wa Jimbo la Vunjo mkoani...
Read more
Mgambo Ashushiwa kipigo na Machinga,Kanisa la Nusuru...
Askari wa Jeshi la Akiba maarufu kama “mgambo” ambaye jina...
Read more
Kuna Ukweli Gani Kuhusu Afya ya Joe...
Rais wa Marekani, Joe Biden amesema ni "Mungu Mwenyezi" pekee...
Read more
SUALA LA PACOME NA CAREN SIMBA LIKO...
NYOTA WETU
See also  Etinosa Idemudia defends Phyna against critics after she mistakenly called out soft drink brand
Mrembo Caren Simba amejikuta kwenye wakati mgumu wa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply