MICHEZO
Majina ya Makocha Thomas Frank wa Brentford na Vincent Kompany wa Burnley yamekuwa ya kwanza kutajwa katika mpango wa kurithi nafasi ya Mauricio Pochettino huko Chelsea.
Uongozi wa Klabu ya Chelsea umetangaza kuachana na Kocha Mauricio Roberto Pochettino Trossero kwa makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja Mkataba ambao ulisainiwa mapema msimu wa 2023/24.
Kocha huyo alisaini mkataba wa miaka miwili, hivyo sehemu ya mwaka mmoja katika Mkataba wake ndio imevunjwa kwa makubaliano maalum yaliyofikia kati yake na Uongozi wa juu wa Chelsea.
Taarifa iliyochapishwa na Gazeti la The Guardian imeeleza kuwa Uongozi wa Chelsea umeanza kujipanga katika mchakato wa kumsaka Kocha Mkuu Mpya, huku ukiamini Thomas Frank wa Brentford na Vincent Kompany wa Burnley watapata upinzani kutoka kwa makocha wengine watakaopendekezwa kurithi mikoba ya Pochettino
Aidha, Gazeti la The Telegraph limeongeza kuwa meneja wa Stuttgart Sebastian Hoeness, Michel wa Girona, Kieran McKenna wa Ipswich na Enzo Maresca wa Leicester wataingizwa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.