TABIA 15 ZA WANAWAKE WALIOPOTEZA SIFA ZA KUOLEWA

0:00

MAPENZI

TABIA 15 ZA WANAWAKE WALIOPOTEZA SIFA ZA KUOLEWA.

1.Mwanamke anaelaumu kwa kila kitu hata umfanyie zuri lipi bado atalaumu. Huona mabaya tu, hana zuri kwake.

2.Mwanamke anayejiona amekamilika, anajihisi anaweza kufanya lolote bila mwanaume, na kuhisi anaweza kufanya lolote analofanya mwanaume, daima anataka haki sawa na hana muda wa kumheshimu mwenza wake.

3.“The Crybaby” Huyu silaha yake ni machozi tu saa zote. Hana namna nyingine ya kuelezea matatizo yake zaidi ya kulia. Muda wote anataka kuonewa huruma, kubembelezwa masaa 24, hana furaha muda wote! Mwanaume huona bora asioe kuliko kuoa mwanamke mwenye sifa hizi.

4.Mzuri Usoni, Muonekano mzuri, ila kichwani hamna kitu, mwanamke wa aina hii hujali tu muonekano wake, na hiyo ndio silaha yake na kujiona malaika! Hana mipango yoyote kimaisha. Japo wanaume wanapenda wanawake wenye muonekano mzuri, kuna muda huhitaji mwanamke anyeweza kupanga nae maisha,

5.Haachi Utoto, na kutotaka kuwa mtu mzima. Sio kila mwanaume anapenda jukumu la malezi kwa mpenzi wake! Japokuwa kuna kipindi mwanaume anaweza kupenda tabia hiyo, ila baadae huchoka kuwa “baba” na kuhitaji kuwa mpenzi na hapo ndipo shida huibuka.

6.Mwanamke Mbinafsi. Daima anataka afanyiwe mazuri yote yeye tu, Mchoyo na hapendi ndugu wa mpenzi wake, pia hayuko tayari kuona mpenzi wake anamsaidia mtu mwingine!

7.Mwanamke anayehisi anawajua wanaume kupita kawaida. Aina hii ya wanawake huhisi wanadanganywa muda wote, hawana muda wa kuwa serious na mahusiano kwa kuhisi wataumizwa kwa kuwa eti “Wanaume wote ni sawa”

8.Mwanamke anaeongea kupita kiasi! Hutaka kumwambia mpenzi wake kila kinachofanywa na watu wengine (Mmbea) hatulii, na mara kadhaa humtia aibu mpenzi wake kwa kuongea ujinga sehemu pasipofaa

9. Mbishi/mbishani….yani hawezi fanya kitu alichoambiwa na boy wake akifanye on time lazima mbishane kwanza hata kama hakina madhara..
Kiufupi wanaume hatupendi kubishiwa hovyo

10. Mwenye kiburi. ..yani ukimwambia ukweli anachukia na anakununia yani hadi tena umbembeleze au umpe kitu ambacho alikua anataka umfanyie. ..

11. Mgumu kuomba MSAMAHA…yani hata akikosea kuomba kwake msamaha ni kugumu sana ….yani yeye anataka akikosea usimwambie unyamaze tu

12.MAPAMBO, anaejipamba kwa mapambo mengi feki…
Mfano; nywele feki, kucha feki, kope feki, mdomoni malips stick kila siku mara meusi mara ya blue mara mekundu. ….
mikucha mirefu yenye rangitofauti
Kiufupi Wanaume tunapenda mwanamke simple ambae hata bila make up anajiamini…mdomoni apake lip shine tu inatosha…

13. IBADA ,Asiyejali maswala ya kumuamini na kumuabudu MUNGU..
yani yeye msikitini hapajui wala kanisani hapajui….hajui kumuomba mungu wala issue za mambo ya kiroho hazipo kabisa kwenye ufahamu wake…yeye daily ni kuweka STATUS za vijembe kwenye whatsap yake na kupost post za vijembe Facebook…na weekend anawaza tu kwenda kujirusha viwanja

14. Anaependa kujipost kila siku mitandaoni akiwa na mapozi ya kimalaya…na mavazi ya ajabu…Mara ajibinue…mara atoe ulimi nje ….mara akae nusu utupu. …mara aoneshe mapaja yake…

15. Ambae HUWAJALI zaidi na kuwapendelea wazazi wake,ndugu zake,jamaa na marafiki zake zaidi kuliko upande wa mwanaume…

See also  WHY AFRICAN COUPLES ARE NOT ROMANTIC

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Presidential jet: Tinubu, NASS, political class now...
Former Minister of Education, Oby Ezekwesili, has said President Bola...
Read more
10 THINGS MEN WANT TO HEAR FROM...
LOVE ❤ 1. "I LOVE YOU" Yes, men like to...
Read more
10 BUSINESS IDEAS FOR STAY HOME MOTHERS.
Stay-at-home mothers have a unique opportunity to explore business ideas...
Read more
Genoa sack Gilardino, Vieira tipped as replacement
Genoa have parted ways with coach Alberto Gilardino, the Serie...
Read more
YUSUPH MANJI AIBUKA AMTAJA KIGOGO ANAYEFANYA SIMBA...
MICHEZO “Unajua wakati nikiwa Yanga, mtu pekee aliyekuwa ananipa wakati...
Read more

Leave a Reply