Jacob Zuma awalalamikia majaji kumzuia kugombea Ubunge

0:00

4 / 100

HABARI KUU

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma amewalalamikia majaji waliotoa uamuzi wa kumzuia kuwania ubunge katika hukumu walioitoa Jumatatu.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu mahakama kumpiga stop kugombea, Zuma ameiambia BBC kwamba Mahakama ya Kikatiba ilikosea kutoa uamuzi kwamba hafai kugombea, kutokana na hukumu dhidi yake ya mwaka 2021 iliyomwona ana hatia ya kudharau mahakama.

“Nilitarajia hilo kutoka kwa majaji, lakini kwa hakika hawako sahihi hata kidogo,” mzee huyo wa miaka 82 amesema, akisisitiza kwamba katiba inapaswa kubadilishwa.

Kabla ya uchaguzi mkuu wa wiki ijayo, Zuma alikuwa akifanya kampeni chini ya bendera ya chama kipya kilichoundwa cha Umkhonto weSizwe .

Alijiunga na chama hicho baada ya kutofautiana na chama tawala cha African National Congress (ANC), alichowahi kukiongoza.

Tume ya Uchaguzi nchini humo ilisema kuwa katiba inamzuia mtu yeyote ambaye alihukumiwa kifungo cha zaidi ya miezi 12 kuhudumu kama Mbunge, ujumbe ulioungwa mkono na Majaji wa Mahakama ya kikatiba.

Zuma alipatikana na hatia mwaka 2021 kwa kukataa kutoa ushahidi wake kwenye uchunguzi wa ufisadi wakati wa uongozi wake.

Mawakili wake walikuwa wamesisitiza kuwa ana haki ya kuwa mbunge kwani kifungo chake kilipunguzwa hadi miezi mitatu baada ya Rais wa sasa, Cyril Ramaphosa kumwachia kutoka gerezani kwa kile kilichoonekana kuwa ni jaribio la kuwatuliza wafuasi wa rais huyo wa zamani waliokuwa na hasira.

“Majaji wa Mahakama ya Kikatiba wamenifanyia mzaha sana. Hawazingatii matakwa ya watu wa nchi hii, wanatumia mapenzi yao wenyewe,”

amelalamika Zuma.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

HOW TO APPROACH A WOMAN
Have confidence; not pride. Confidence is attractive, women detest pride.
See also  Kwanini Obama na Michelle Wanamuunga Mkono Kamala?
Women...
Read more
CHAMA NA KAPAMA WASIMAMISHWA SIMBA ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye Jamhuri yetu tukufu...
Read more
SAFARI YA ZITTO KABWE KUGOMBEA URAIS WA...
HABARI KUU Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa...
Read more
Idadi ya Waandamanaji waliofariki Kenya Mpaka Sasa
Waandamaji zaidi ya Watano wameuwawa kwa risasi wakati Polisi...
Read more
BENJAMIN NETANYAHU KUFANYIWA UPASUAJI KUTOKANA NA TATIZO...
HABARI KUU Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu anatarajia kufanyiwa...
Read more

Leave a Reply