MAKOMBORA YA ANGA YA ISRAEL YAUWA WATU 35 UKANDA WA GAZA

0:00

HABARI KUU

Duru za ndani nchini Israel zinasema serikali ya taifa hilo itatoa karipio kali kwa mabalozi wa Ireland, Norway na Uhispania kutokana na mpango wa serikali zao wa kulitambua taifa la Palestina juma lijalo.

Taarifa hiyo inatolewa wakati ndani ya Ukanda wa Gaza Wapalestina 35 wakiripotiwa kuuwawa kwa mashambulizi ya jeshi lake usiku wa kuamkia leo.

Mabalozi hao wameitwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Israel, ambapo pamoja na masuala mengine wataoneshwa vidio ambazo hazijaoneshwa hadharani za Hamas wakiwachukua mateka wanawake wakati wa shambulio la Oktoba 7 kwa Israeli ambalo lilizusha vita vya Gaza.

Israel pia imewaita tena mabalozi wake huko Dublin, Oslo na Madrid kwa mashauriano.

Akizungumzia suala la utambuzi wa taifa la Palestina Waziri wa Mambo ya Nje wa Colombia, Luis Gilberto Murillo amesema wanaamini na wana uhakika kwamba nchi nyingi zaidi zitaitambua Palestina ingawaje Umoja wa Mataifa uliridhia, katika muktadha wa Makubaliano ya Oslo, kwamba suluhisho la serikali mbili linapaswa kuundwa.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MBAPPE KUONDOKA PSG ...
MICHEZO Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe amefikia makubaliano...
Read more
Kongamano la Uswizi: Putin na Utata wa...
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Ukraine itahitaji kuondoa kikamilifu...
Read more
WILL SMITH NDOA YAKE IMEMSHINDA ...
NYOTA WETU Muigizaji na mtangazaji Jada Pinkett Smith ameweka wazi kuwa...
Read more
Yul Edochie’s ex-wife, May, joins Nollywood
May, the estranged wife of Nollywood actor Yul Edochie, has...
Read more
China Shine in Paralympic Powerlifting as LingLing...
CHINA’S women dominated the first day of powerlifting at the...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  Katibu Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Ado Shaibu amesema kuwa kinachoendelea katika Uchaguzi Mkuu nchini Afrika Kusini ambapo Chama Tawala cha ANC kimeshindwa kupata kura za kuunda serikali peke yake inapaswa kuwa somo kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Leave a Reply