Mshambuliaji wa KMC Wazir Junior ameitwa katika kikosi cha timu ya taifa Tanzania kinachojiandaa na mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Zambia.
Kikosi hicho cha kocha Hemed Seleman kitaingia kambini Juni Mosi kujiandaa na mechi hiyo, huku wachezaji wa Yanga SC na Azam FC wakitarajiwa kujiunga na kambi hiyo baada ya kumaliza mchezo wao wa Fainali ya FA.
Kikosi hicho kina makipa Ally Salim, Aboutwaleeb Mshery
Yonna Geoffrey na Kwessi Kawawa.
Mabeki ni Haji Mnoga, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim HamadNickson Kibabage, Mohamed Hussein, Lameck Lawi Israel Mwenda, Mukrim Issa, Lusajo Mwaikenda, Pascal Msindo na Nathaniel Chilambo.
Viungo ni Novatus Dismas, Yussuf Kagoma, Morice Michael, Yahya Zaydi, Himid Mao, Feisal Salum na Mudathir Yahya.
Washambuliaji ni Abel JosiahEdwin Balua, Saimon Msuva
Kibu Denis, Cyprian Kachwele,Ben Starkie, Charles M’mombwa, Ibrahim Hamad, Kelvin John, Abdul Suleiman na Clement Mzize