SABABU ZA JESHI KUONGEZA MUDA WA UTAWALA BURKINA FASO

0:00

4 / 100

Utawala wa Kijeshi wa Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye aliingia Madarakani Septemba 2022 kupitia Mapinduzi ya Kijeshi, atarefusha kipindi chake cha uongozi wa nchi kwa miaka mitano zaidi, kulingana na katiba iliyopitishwa Jumamosi na washiriki katika mikutano ya Kitaifa huko Ouagadougou.

“Muda wa mpito umewekwa kuwa miezi 60 kutoka Julai 2, 2024,” alisema Kanali Moussa Diallo, Rais wa Kamati ya maandalizi ya mikutano .

Rais Traoré pia ataweza kusimama katika chaguzi za Urais Ubunge na Manispaa ambao utaandaliwa ili kukomesha mpito”, aliendelea kusema Kanali Diallo.

Mikutano hiyo ya kitaifa, iliyopangwa kumalizika Jumapili, ilileta pamoja wawakilishi wa mashirika ya kiraia, vikosi vya ulinzi na usalama na hata manaibu kutoka bunge la mpito siku ya Jumamosi. Vyama vingi vya kisiasa vilisusia hafla hiyo.

Utawala wa mpito ulipaswa kumalizika Julai 1, 2024, lakini mara kadhaa Kapteni Traoré alizungumzia ugumu wa kufanya uchaguzi kutokana na mazingira ya usalama nchini.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

WAFANYABIASHARA WAMUOMBA RAIS TINUBU KUWAPA WANAJESHI WA...
HABARI KUU Muungano wa wafanyakazi wa mafuta nchini Nigeria umemuomba...
Read more
SIMBA YATAMBA KUPIGA KWENYE MSHONO
MAGAZETI Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
USIFANYE MAKOSA HAYA UNAPOKUWA KWENYE MAHUSIANO ...
Makala Fupi Kilio cha wengi walio kwenye mahusiano ni kuhisi wanasalitiwa...
Read more
Kongamano la Uswizi: Putin na Utata wa...
Rais wa Urusi Vladimir Putin amesema Ukraine itahitaji kuondoa kikamilifu...
Read more
Rais Samia atoa ujumbe mzito kwa viongozi...
Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo kwenye...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  7 Insane Things you must know about Girls:

Leave a Reply