Kwanini Patrice Motsepe alisema goli la Young Africans lilikuwa halali?

0:00

4 / 100

Ijumaa iliyopita Asubuhi Rais wa CAF, Patrice Motsepe alikuwa katika ardhi ya Tanzania Visiwani Zanzibar. Motsepe alikuja kwa ajili ya Mashindano ya Fainali za African Schools Football.

Baadae muda mfupi tukaona stori ikitembea mitandaoni kuwa Motsepe amekubali bao alilofunga Stephane Aziz KI pale kwa Madiba dhidi ya Mamelodi Sundowns lilikuwa bao halali.

Ni kichekesho, Kwanini Motsepe atoe kauli hii leo? Kauli yake haina madhara yoyote kwa sasa, zaidi inawapaka @yangasc mafuta kwa mgongo wa chupa.

Afrika ilisema, Yanga SC nao waliandika hadi barua kuhusu bao kukataliwa. Kila mmoja alichafukwa kwa kilichotokea usiku ule, lakini barua ya Yanga SC nayo isingeweza kubadili uamuzi wa kiwanjani.

Maisha yalikuwa hivi. Vitu vingi vimepita hapa kati baada ya mechi ile ya Afrika Kusini. Juzi Motsepe amekuja kuishitua mioyo iliyolala. Sijui aliulizwa swali au aliamua ‘kujiropokea’ zake.

Sijui kwanini Motsepe alifanya vile. Kinachomuhukumu Motsepe ni kitu kimoja tu. Nafasi yake ya Urais ndani ya CAF na nafasi yake kama kiongozi wa juu wa Mamelodi Sundowns.

Motsepe amekasimu madaraka yake kwa mtoto wake pale Mamelodi, lakini nyuma ya pazıa ni rahisı hivyo? Mashaka yanaingia unapojua tuko Afrika.

Ni kweli Motsepe hana ushawishi na chochote ndani ya Mamelodi? Swali ni gumu. Jibu lake ni jepesi tu. Afrika bado hatuna utaratibu wa kuachia madaraka na kuacha kufuata guata kwa nyuma.

Mbele ya pazia ni kweli Motsepe hafanyi kazi zozote za Mamelodi. Hii ni nyuma ya pazia, lakini nyuma ya pazia bado Motsepe ana nguvu na ushawishi mkubwa na muda mwingine huenda akawa anapiga hadi simu kuulizia mambo yanavyokwenda.

See also  Erik ten Hag aomba muda zaidi Manchester United

Kiufupi tu, Motsepe ameamua kusema tunachopenda kukisikia. Watanzania wanapenda vile. Kuna Watanzania wameondoka na kauli ile na kusahau kila kitu.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

THE BENEFITS OF KISSING
LOVE TIPS ❤ 15 BEST BENEFITS YOU NEED TO KNOW...
Read more
Footballer Emmanuel Emenike, captured social media with...
Emmanuel Emenike, the former Super Eagles striker, couldn’t help but...
Read more
SABABU TFF KURUDISHA LIGI YA MUUNGANO
MICHEZO Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20 Kombe...
Read more
McLaren right of review over Norris penalty...
MEXICO CITY, - McLaren's petition for a right of review...
Read more
Leverkusen dominate but stumble to goalless draw...
LEVERKUSEN, Germany, 🇩🇪 - Champions Bayer Leverkusen twice hit the...
Read more

Leave a Reply