Rais Jakaya Kikwete kinara wa kutafuta fedha za uwekezaji kwenye Elimu

0:00

4 / 100

Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete kwa nafasi yake ya Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Ubia wa Elimu Duniani (GPE) ameshiriki Mkutano wa Mwaka 2024 wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB 2024 Annual Meeting) unaofanyika jijini Nairobi, Kenya tarehe 26 – 28 Mei, 2024. Ametumia fursa ya kushiriki Mkutano huo kuzungumza na vongozi mbalimbali, hususan kutoka sekta za kifedha, sekta binafsi na washirika wa kimaendeleo kuhusu umuhimu wa kuongeza ufadhili wa kifedha ili kuimarisha mpango wa utoaji chakula kwa wanafunzi wakiwa mashuleni pamoja na kuhamasisha ubunifu wa mbinu mpya za kufadhili elimu ya juu, elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi.

Taasisi ya GPE ambayo Rais Mstaafu Kikwete ni Mwenyekiti wa Bodi imejikita katika kujenga ubia na wadau mbalimbali wa kimataifa na ndiyo Taasisi kinara duniani inayohamasisha jitihada za kuzisaidia nchi zaidi ya 76 kuimarisha mifumo yao ya elimu ili kutoa elimu bora zaidi kwa watoto wa kike na wa kiume, hususan wale wanaotoka katika mazingira duni, wenye ulemavu na wanaoathiriwa na majanga kama vile vita na athari za mabadiliko ya tabianchi.

Kwa upande wa Afrika, GPE ina miradi inayozunufaisha nchi 40, ikiwemo Tanzania. Tangu mwaka 2016 hadi sasa, Taasisi ya GPE imetoa msaada wa zaidi ya shilingi bilioni 250 za Kitanzania kufadhili programu hiyo ya utoaji wa chakula mashuleni katika nchi inapofanya shuhuli zake.

Katika Mkutano huo, pamoja na mambo mengine, Rais Mstaafu Kikwete alieleza umuhimu wa washiriki kufikiria mbinu mpya za kupata fedha zitakazotumika kugharamia programu za kutoa chakula mashuleni kwani ukweli ni kwamba licha ya jitihada kubwa inayofanyika na nchi nyingi za kipato cha chini na kati katika kuimarisha programu hiyo, bado zinakabiliwa na changamoto mbalimbali za kiuchumi ikiwemo kuelemewa na madeni.

See also  Namna Kisukari Kinavyosababisha Upotevu wa kuona

Akaeleza kuwa programu ambayo ni moja ya mikakati muhimu ya kielimu inayoongeza mahudhurio ya watoto mashuleni na kukuza uelewa wa wanafunzi inasaidia pia katika kukabiliana na tatizo la udumavu na unyafuzi linalolikabili bara la Afrika. Aidha, aliwakumbusha washiriki kuwa msingi wa bara la Afrika na Dunia kufikia malengo waliyojiwekea kama vile lengo la Umoja wa Afrika la Ajenda 2063.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MVUA KUBWA KUSHUKA KESHO KWENYE MIKOA MITANO.
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
DIDIER DESCHAMPS AMKATAA WILLIAM SALIBA ...
MICHEZO Baada ya mlinzi wa Arsenal Wiliam Saliba kukosekana katika...
Read more
Kurasa za Magazeti ya leo
Read more
Ukweli Kuhusu Vita ya Israel na Palestine
Taarifa za kuuawa kwa Katibu Mkuu wa Chama cha siasa...
Read more
SIGNS YOU ARE DATING AN ABUSIVE PERSON
Now, when we talk of abuse, a lot of us...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply