CHANZO KIKUU CHA TATIZO LA HARUFU MBAYA UKENI NA TIBA YAKE

0:00

4 / 100

HARI YA ACID YA UKE (VAGINA PH)
PH ni kipimo cha kuonesha jinsi gani kitu Fulani kilivyo na kiasi cha acid au nyongo (base).Kipimo hiki kina viwango 1 mpaka 14.Kiwango cha PH chini ya 7 inamaana hicho kitu kina ACID na juu ya 7 Ina maan hicho kitu ni nyongo (base).Maji yenyewe huwa ni neutral yana PH ya 7 ina maana si acid wala si nyongo.

Vitu hivi vina umuhimu gani kwenye uke.?
Kuelewa PH ya uke wako kama ni Acidic au Basic inakusaidia kufahamu kama uke wako upo katika hali nzuri.Pia inasaidia kupata aina Fulani ya jinsia ya mtoto kwa mbegu za kiume X na Y zipo zinazostahimili hali ya acid na zipo zinazostaimili hali ya nyongo (basic) kama tutavoona.

UKE UNAPASWA UWE NA PH YA NGAPI?
Kikawaida uke unapaswa kuwa na PH kati ya 3.8 hadi 4.5,Japo kuwa inaweza kubadilika kutokana na umri. Kwa mfano kwa wanawake walio kwenye umri wa kuzaa (miaka 15 hadi 49) PH ya uke inapaswa iwe 4 hadi 4.5 ila siku chache kabla ya hedhi na baada ya ukomo wa hedhi inaweza kuwa Zaidi ya 4.5.
Kwa nini PH ya uke kuwa ndogo ina umuhimu.
Kama tulivyoona PH ndogo inamaanisha Acid,hali ya uke kuwa na PH ya Acid inaukinga uke, inasaidia kuzuia wadudu bakteria na fangasi kukua kwa kasi na kusababisha magonjwa kama Fangasi za ukeni.
Uke ukiwa na PH kubwa kama tulivoona inayoelekea kwenye nyongo (base)/Zaidi ya 5 Inatengeneza mazingira mazuri ya bakteria na fangas wa ukeni kukua kwa kasi bila mpangilio na kusababisha matatizo ikiwemo harufu mbaya ya uke

Kuwa na PH kubwa inakuweka kwenye hatari ya kupata matatizo yafatayo:
BACTERIAL VAGINOSIS
Ni hali inayotokana na kukua kwa kasi na bila mpangilio kwa bakteria kwenye uke ,hali hii hupelekea harufu mbaya ukeni inayokuwa kama shombo la samaki aliyeharibika,ikiambatana na ute wa kijivu mweupe au wa njano.Pia inaweza kuambatana na muwasho ukeni na maumivu wakati wa kukojoa, pia maumivu wakati wat endo la ndoa. Tatizo hili kwa mwanamke humweka kwenye hatari (risk) ya kupata maambukizi kama ya Human Papilloma virus (HPV) kirusi kinachosababisha saratani ya shingo ya kizazi, Herpes simplex na HIV.

TRICHOMONIASIS
Huu ni ugonjwa wa zinaa unaosababishwa na Bakteria wanaojulikana kama Trichomonas vaginalis.Kwa wanawake wengi wanapopata ugonjwa huu hawapati dalili zozote. Ila wanapopata dalili huwa kama ifatavyo
1.harufu mbaya ukeni
2.Ute wa kijani au njano
3.muwasho ukeni unaoenda hadi sehemu za juu za mapaja.

See also  HOW TO MAKE YOUR WIFE RESPECT YOU IN THE MARRIAGE

JE PH YA UKE IWA CHINI SANA INA MADHARA?
Kama tulivyoona kikawaida uke wenye afya nzuri unapaswa kuwa na PH kati ya 3.8 hadi 4.5.
Ukiwa na PH chini ya 3.8 (more acidic) Haisababishi magonjwa ila inapunguza uwezo wa kushika mimba. Kwani mbegu za kiume zinaweza kustaimili PH ya kawaida sawa na maji yaani PH kati ya 7.0 hadi 8.0 ndio maana wakati wat endo la ndoa uke utengeneza ute ili kuongeza PH ya uke mbegu zikiingia zisife.pia Majimaji yanayotangulia kutoka kwa mwanaume (semen) huwa na kzai hiyo pia kupunguza hali ya acid ya uke.
Kwa hiyo Asidi ikizidi kwenye uke basi hupelekea mbegu kufa zikiingia kwenye uke.

VITU GANI VINASABABISHA PH YA UKE KUTOKUWA SAWA
1.Kufanya mapenzi bila kinga
Majimaji yanayotangulia kabla ya mbegu za kiume huwa na hali ya nyongo (basic) yakiwa na lengo la kupunguza hali ya aside kwenye uke ili kutengeneza mazingira rafiki kwa mbegu za kiume. Kwa hiyo maji maji haya husababisha PH ya uke kuongezeka wakati wat endo
2.Madawa ya kuua Bakteria (ant biotics)
Dawa hizi ndio maana hazishauriwi kutumika kiholela.Kwani mabli na kuua Wadudu wanaosababisha magonjwa pia zinaua na bakteria wazuri wanaosaidia kuweka hali ya uke katika usawa.
3.Kusafisha uke hadi ndani.
Uke siku zote unajisafisha, uchafu uliopo kwa ndani hujisogeza hadi juu kwenye uke ili usafishwe. Unaposafisha uke kwa kuingiza kidole hadi ndani inasababisha kuondoa usawa wa PH ya uke. Ndo sababu unaambiwa kusafisha hivyo inapelekea kupata magonjwa kama fangasi za ukeni nk. Kwa inasababisha kuongezeka kwa PH ya uke.
4.Hedhi
Damu inapokua inapita kwenye uke wakati wa hedhi inapelekea PH ya uke kuongezeka. Pia mabadiliko ya hormone hasa estroigen pia hupelekea PH ya uke kuongezeka na kupoteza hali ya aside ya kawaida ukeni. Ndo maana wengine mara nyingi anapokua katika kipindi hiki au siku chache baada ya kumaliza wanapata matatizo kama Fangasi za ukeni,UTI nk

DALILI ZA PH YA UKE KUWA JUU/KUPOTEA KWA HALI YA ASIDI YA UKE
Harufu mbaya ukeni, inaweza kuwa kama shombo la samaki alieharibika
Ute wa kijivu, mweupe au njano
Muwasho ukeni
Maumivu wakati wa kukojoa

JINSI GANI YA KUONDOA TATIZO HILI
1.Epuka kusafisha uke hadi ndani
Sawa utaona inaondoa uchafu,ila haikusaidii bali inaondoa Zaidi hali ya Asidi ya uke na kupelekea kuongeza tatizo la harufu mbaya ukeni

2.Pata matibabu ya Bacteria vaginosis
3.Kunywa mtindi.
Mtindi una bakteria wazuri wanaosaidia kuweka uke katika hali yake wanajulikana kitaalamu kama PROBIOTICS.Unapokunywa mtindi inasaidia kuweka hali ya uke katika usawa na kukukinga na magonjwa kama fangasi za ukeni na vaginosis

See also  Chaos at JKIA: Union Workers Strike Over Adani Takeover Plan

MAMBO MENGINE YA KUZINGATIA
VAA NGUO ZA NDANI ZENYE ASILI YA PAMBA(COTTON)
Pamba(cotton) ina uwezo wa kupitisha hewa hata kama ni kidogo sana. Na sehemu za siri za Mwanamke zinahitaji flow ya hewa inayopita,nyingine iwe inaingia na nyingine iwe inatoka.Hii flow ya hewa hata kama ni ndogo itasaidia kufanya sehemu zako za siri kuwa fresh muda wote na utapunguza uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.
Na pia punguza kuvaa nguo za kubana sana muda wote,nguo za kubana zinasababisha majasho sehemu za siri na ukizingatia hamna flow ya hewa kwenye sehemu zako za siri basi lazima hayo majasho yataanza kutoa harufu mbaya.

4.USIVAE NGUO YA NDANI MOJA SIKU NZIMA
Kwa jinsi maumbile ya Mwanamke yalivyo,unatakiwa kubadili nguo ya ndani mara mbili au tatu kwa siku.
May b ulivaa nguo ya ndani asubuhi,ikifika mchana,ingia ladies room(bafuni/chooni),Vua Nguo yako ya Ndani,kisha unaweza ukaoga mwili mzima(which is better) au ukasafisha sehemu zako za siri.Nguo ya ndani uliyovua unaweza ukaifua(which is better) au ukaikunjakunja na kuiweka ndani ya kipande cha khanga au kitenge ndio uweke kwenye handbag yako ili kama ikitokea ukaopen handbag yako in public,watu wataona khanga au kitenge,hawatojua ndani umeweka nini.

5.PUNGUZA KULA VYAKULA VYENYE SUKARI AU YEAST KWA WINGI
Unaweza ukapunguza uwezekano wa kupata Yeast Infection au Bacteral Vaginosis kwa kuacha au kupunguza kula vyakula vyote vyenye sukari au yeast kwa wingi.
Vyakula hivyo ni kama vile vyakula vyote vinavyotengenezwa na hamira,pombe/bia n.k
Ukizidisha Vyakula au vinywaji hivi,ina maana utakuwa unazidisha yeast mwilini,na wakizidi kwenye uke utapata yeast Infection,mwisho wake uke wako utaanza kutoa harufu mbaya.

6.BADILI PADS ZAKO MARA KWA MARA UNAPOKUWA KWENYE SIKU ZAKO
Ili kuzuia uke wako usitoe harufu mbaya kipindi ambacho upo kwenye siku zako,inashauriwa kubadili ur pad mara kwa mara(may b after each 4 or 6 or 8 hours,it will depend how many pads can u afford per day)
Kubadili pads mara kwa mara kunasaidia ujisikie upo comfortable,inazuia bacteria kujikusanya,inasaidia kupunguza uwezekano wa kupata infection na mwisho inaondoa uwezekano wa uke wako kutoa harufu mbaya.

MATIBABU YA NYUMBANI.
Endapo unasumbuliwa mara kwa mara na Tatizo la harufu ukeni, au unapata matatizo kama fangas za ukeni mara kwa mara na UTI zingatia hapa.
Bilas haka umesikia mengi mfano,
Kuweka limao ukeni
Kuweka kitunguu saumu
Kuweka Bicarbonate nk.
Ila ukweli ni kwamba Unachohitaji ni kuweka PH ya uke wako kati ya 3.8 hadi 4.5 ndo itakua suruhisho la tatizo lako. Kama tayari umeshapata Fangas za ukeni au Bakteria vaginosis inapaswa Upatiwe matibabu kwanza ndo ubalance PH ya uke ili kuzuia tatizo lisitokee tena.

See also  BOVI JOKES ABOUT HIS WIFE DECEIVING HIM INTO MARRIAGE

KUHUSU LIMAO
Wengi hudai Kwamba limao au kuweka juisi ya limao ukeni inatibu fangasi za ukeni na inatibu Fangasi na UTI.
Limao haitibu fangasi wala bakteria. Limao ndani yake ina Asidi ya PH ya 4.2, Tafiti zinaonesha unapoweka juisi hii kwenye uke inaongeza PH kwa kiwango cha 0.2 zaidi. Ila Limao ina vitu vingine ndani yake.Inapomeng’enywa viambata vyake vinapovunjwa vunjwa vinatengeneza end products ambazo zina PH ya 8.9 yaani Hali ya nyongo (basic) hivyo kupandisha tena PH ya uke. Pia unapokunywa juice yake inapofikia kutolewa kwenye mkojo huwa si aside tena inaongeza PH ya mkojo. Kwa hiyo juice ya limao unapoiweka ukeni Katika dakika za mwanzo inaopunguza PH ya uke kwa 0.2 yaani kama iliku 7.2 itakua 7 na kuendelea ila baada ya muda bakteria wa ukeni wanapoanza kuivunja vunja inaongeza PH hadi 7.5 hadi 8.5. Kwa hiyo haisaidii.

KUHUSU BICARBONATE NA KITUNGUU SAUMU
Kwa kuanza na kitunguu saumu ndani yake kina Allicin hiyo inayokipa harufu yake.Allicini ni nyongo (base) ina PH ya 7.9, hivyo inapotumika haisaidii bali I naongeza tu PH ya uke kuwa Basic
Bicarbonate yenyewe hii pia ni nyongo,ukiweka unaongeza PH ya uke na kuongeza hali ya nyongo (basic) ya uke hivyo kuzidisha tatizo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MICHUANO YA AFRICON YAFUNIKA KIBIASHARA
MICHEZO Rais wa Shirikisho la mpira wa miguu Afrika (CAF)...
Read more
KURASA ZA MAGAZETI YA LEO YA TANZANIA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MALAM BACAI SANHA JR AHUKUMIWA MIAKA 6...
HABARI KUU Mahakama nchini Marekani imemuhukumu kifungo cha zaidi ya...
Read more
𝘽𝙪𝙨𝙞𝙣𝙚𝙨𝙨 𝙋𝙖𝙧𝙩𝙣𝙚𝙧𝙨𝙝𝙞𝙥𝙨; 𝙩𝙝𝙞𝙣𝙜𝙨 𝙮𝙤𝙪 𝙣𝙚𝙚𝙙 𝙩𝙤 𝙠𝙣𝙤𝙬...
For us to properly discuss partnerships, we must first define...
Read more
KINZUMBI YANGA MUSONDA MAZEMBE
MICHEZO YOUNG AFRICANS KAZI KWENU SASA. Tunafahamu kuwa klabu ya Yanga...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply