Familia ya Mpanda Milima, Joshua Cheruiyot Kirui, aliyefariki wakati akipanda Mlima Everest Mei 22, 2024, imesema Mwili huo utaachwa alikofia kutokana na gharama na hatari za mchakato wa kuurejesha mwili wake nchini humo
Cheruiyot alianguka kwenye Ufa uliopo umbali wa Mita 48 kutoka kwenye Kilele cha mlima huo wenye Mita 8,848.86 ambapo imeelezwa kuurejesha mwili wake kutoka umbali huo itakuwa ni hatari kwa timu ya uokoaji, na familia haipo tayari kuhatarisha maisha ya wengine
Inakadiriwa kuwa karibu miili 200 kati ya wapandaji 330 waliofariki kwenye mlima Everest ambao ndio mrefu zaidi duniani, bado ipo katika eneo hilo
Inaelezwa kuwa gharama za kuurejesha mwili ni Ksh. Milioni 9 (takriban Tsh. Milioni 178) na itahitaji Watu 8 kupanda juu na kubeba mwili huo. Kutokana na hilo, Familia nyingi zinazopoteza wapendwa wao huamua kuwaacha huko