MFAHAMU MCHEZA FILAMU ZA NGONO STORMY DANIELS ANAYEMTESA DONALD TRUMP

0:00

10 / 100

Stormy Daniels ndilo jina la mwanamke aliyetawala katika kesi ya jinai ambayo Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump alipatikana na hatia katika kesi ya kihistoria iliyofanyika Manhattan.

Jina lake halisi ni Stephanie Gregory Clifford, mwigizaji wa zamani na mkurugenzi wa filamu za wakubwa. Katika kesi hiyo anadai kuwa mwaka 2006 alikutana na Trump, wakati tayari alikuwa ameoana na mke wake wa sasa, Melania, kitu ambacho mara kwa mara Trump alikanusha.

Majaji wa mahakama ya New York wameonekana kumwamini na hivyo kumpata rais huyo wa zamani wa Marekani na hatia ya mashtaka 34 yanayohusiana na kughushi taarifa za uhasibu ili kuficha malipo ambayo wakili wa Trump angemlipa mwanamke huyo ili kununua ukimya wake kuhusu uhusiano huo na hivyo kumlinda katika kampeni za uchaguzi za mwaka 2016 ambazo Trump alishinda urais.

Stephanie alizaliwa Baton Rouge, katika jimbo la kusini la Louisiana, mwaka wa 1979, na ni mpenzi wa kuendesha farasi.

Akiwa mtoto, ndoto yake ilikuwa kuwa daktari wa mifugo, lakini baada ya talaka ya wazazi wake akiwa na umri wa miaka minne, alilelewa na mama yake ambaye alikuwa na wakati mgumu kumsomesha.

Katika umri wa miaka 17 alianza kufanya kazi kama mcheza dansi katika vilabu vya usiku.

Mwaka 2000 alianza kazi yake kama mwigizaji wa filamu za watu wazima na kampuni ya utengenezaji wa Wicked Pictures.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini Mwabukusi Ameenguliwa Kwenye Uchaguzi wa TLS?
Kamati ya uchaguzi ya Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) imeengua...
Read more
REVEALING SIGNS YOUR WIFE IS IN LOVE...
In addition to all these, sexuality is of great importance...
Read more
Erik Ten Hag atoa maoni yake juu...
MICHEZO
See also  Billionaire Adedeji Adeleke on his Davido’s daughter birthday
Kocha wa Klabu ya Manchester United, Erik Ten Hag...
Read more
Kenyan Immigration Simplifies Passport Collection Process
The Directorate of Immigration Services in Kenya has announced the...
Read more
Duale Defends Military Deployment During June 2024...
In his vetting as the nominee for Environment Cabinet Secretary,...
Read more

Leave a Reply