TANZANIA YAZINDUA MAGARI YA UMEME

0:00

8 / 100

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amezindua magari yanayotumia mfumo wa umeme ikiwa ni jitihada za Serikali za kuwezesha wananchi kutumia nishati safi nchini.

Uzinduzi wa magari hayo umefanyika leo Mei 30, 2024 jijini Dodoma sanjari na uzinduzi wa Ofisi za Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) pamoja na kituo cha uzalishaji wa umeme wa jua.

“Niwapongeze wadau wetu kutoka Umoja wa Ulaya (EU) na Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) kwa hatua hii, mtakumbuka kwamba Serikali inaendelea kutafuta mbadala wa kuwawezesha wananchi hasa wale walio na uhitaji zaidi wa nishati safi”, amesema Dkt. Biteko.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa wadau wanaoshirikiana na Serikali kutafuta uwezekano wa kuwa na nishati safi ya uhakika ili kufikia malengo ya asilimia 80 ya Watanzania kutumia nishati safi ifikapo 2034.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa UNDP, Bi. Weyinmi Omanuli ameipongeza Serikali kwa hatua zinazoendelea kuelekea kuwawezesha wananchi wake katika nyanja mbalimbali kijamii na kiuchumi.

Amesema kuwa kampeni ya Nishati Safi ya kupikia imekuwa kielelezo thabiti cha Serikali kuwajali wananchi wake hususani wale wa kipato cha chini.

Naye, Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya, Bw. Cedric Marel amesema Umoja huo una imani kubwa na Serikali kupitia Wizara ya Nishati kuendeleza jitihada za kuwakomboa wananchi kwa kuandaa mazingira wezeshi yanayolenga kuboresha maisha yao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Magoma na Yanga Ngoma Nzito
Mzee Magoma ameamriwa na mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu kuilipa...
Read more
ABIBATU MOGAJI THE PLAY
President Bola Tinubu spoke at a stage production held in...
Read more
ARSENAL WAPO KILELENI MWA MSIMAMO WA LIGI...
MICHEZO
See also  DE BRUYNE NA MANCHESTER CITY BADO NGOMA NZITO
Bao la dakika za jioni kabisa la Kai Havertz...
Read more
ALIYEUWA NDUGU WAWILI KUNYONGWA
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Mkuu wa Wilaya atoa Dau kwa Atakayempa...
Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti ametangaza dau la...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply