Bondia wa Tanzania Hassan Mwakinyo ametoa ufafanuzi kuhusu pambano lake dhidi ya Patrick Allotey kutoka nchini Ghana juzi usiku.
Related Content
Mwakinyo ameshindwa kucheza pambano hilo kutokana na kushindwa kukamilika kwa baadhi ya taratibu za pambano.
Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram @hassanmwakinyojr ameanza kuandika kuwa… “ Guys naomba niombe radhi mashabiki wangu wote na niweke wazi kwenu kitu kimoja kulingana na sitofaham iliyo tokea juzi kwa mimi kutocheza kwenye pambano langu lilo tarajiwa na wengi wenu, NAOMBA NIANDIKE KWA HERUFI KUBWA YA KWAMBA AZAM TV HAWANA CHUKI WALA BIFU YOYOTE NA MIMI kama inavyo tafsiriwa na wengi binafsi kilichotokea juzi wamejitahidi sana kupambana kisitokee nimeona jitihada zao kubwa sana zikifanyika kunusuru lile pambano kuanzia ngazi za juu mpaka chini ya uwongozi, yani hata kulipokua na taarfa ya pambano kufutwa na uwongozi wa chama cha ngumi ilikuwa ni Sawa kabisa kulingana walishaona kuna mapungufu mengi ambayo walijua yangetokea haya’ anyway kiufupi ipo haja sasa ya sisi wapiganaji kupewa fursa na kipaumbele cha kufanya kazi kupitia promoshen zetu hii itasaidia kuepeusha matatizo ya lazima yanayo węża kujitokeza kwa mapromoter wahuni waongo kama ilivyotokea na ni vile.
sasa nimekua nafikiri zaidi kabla ya kufanya kitu lakini kama nisingefanikiwa kupigana lile pambano jana kwa jitihada zangu binafsi basi huwenda sasa ningekuwa ostabey police kwa jinai Mbaya kubwa Ambayo pengine ingepumbazisha fikra na akili ya kila ambae angeskia kuhusu all in all nawashukuru sana mashabiki zangu ambao hawakusita kufika na kuungana na mimi na wote ambao wamekua wakifuatilia wakati wote Mwenyez Mungu atawalipa zaidi ya mapenzi yenu…..”
Related Content