Kiongozi wa upinzani Nchini Israel Yair Lapid ametoa wito kwa Waziri Mkuu wa taifa hilo Benjamin Netanyahu, kuzingatia mpango uliotangazwa na rais wa Marekani Joe Biden wa kusitisha mapigano Gaza.

0:00

9 / 100

Lapid ametoa pendekezo la kuiunga mkono serikali iwapo washirika wa serikali ya Netanyahu wataukataa mpango huo uliotangazwa na Biden.

Familia za mateka wa Israel wanaoshikiliwa na Hamas wametaka pande zote mbili kuukubali mpango huo wa kumaliza vita vilivyodumu kwa miezi minane sasa na kutaka jamaa zao kurejea nyumbani, lakini Israel imeendelea kusema masharti ya kusitisha mapigano lazima yatimizwe kwanza.

Rais wa Marekani Joe Biden siku ya jana alieleza namna mpango huo wa hatua tatu wa kusitisha mapigano utakavyotekelezwa.

Hatua ya kwanza itakuwa ni kipindi cha wiki sita cha usitishaji mapigano ambacho kitashuhudia vikosi vya Israel vikiondoka kwenye miji yote iliyo na watu wengi kwenye Ukanda wa Gaza.

Kisha itafuatiwa hatua ya pili na ya tatu inayojumuisha kubadilishana mateka wote na wafungwa, na baadae vikosi vya Israel vitaondoka kikamilifu na mpango wa kuijenga upya Gaza utaanza..

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kwanini Yanga ilimhitaji zaidi Chama kuliko Simba?
UCHAMBUZI Faida ya uwepo wa Chama Jangwani kwanza uzoefu wa mashindano...
Read more
The founder of Christ Mercyland Deliverance Ministry,...
VeryDarkMan made this known on Thursday, in a now trending...
Read more
MBAPPE KUONDOKA PSG ...
MICHEZO Mshambuliaji wa Paris St-Germain Kylian Mbappe amefikia makubaliano...
Read more
BABA WA LUIS DIAZ AMEREJESHWA ...
NYOTA WETU. Baba Mzazi wa nyota wa Liverpool Luis Diaz...
Read more
Lafey MP Launches Dam and Borehole Projects...
Lafey Member of Parliament (MP) Mohamed Abdikheir has taken a...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  We Are Are Fighting A War — DHQ Opens Up On Borno Bombings

Leave a Reply