Aliyekuwa mgombea wa kanda ya Nyasa ya Chadema, Mchungaji Peter Msigwa amekata rufaa katika chama hicho, akidai ushindi alioupata Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ haukuwa halali na kulikuwa na mbinu chafu dhidi yake.

0:00

9 / 100

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatatu Juni 3, 2024 Mkoani Iringa, Msigwa ameonesha kutokubaliana na matokeo akidai kuwa hawezi kushindwa uchaguzi.

“Mimi siwezi kushindwa, mimi uchaguzi huu (Uchaguzi wa uongozi wa CHADEMA kanda ya Nyasa) sikushindwa, tumemchagua mwenyekiti wa uchaguzi anaitwa Ayubu Sikagonamo ni mwenyekiti wa wilaya kule wilaya ya Momba alikuwa timu yetu tukashinda, yule mwenyekiti ndiye ambaye huwa anatoa kura ya turufu, tukashinda kwa tofauti ya kura 59 kwa 49 tulikuwa mbele sisi kura 10 pungufu ya kura tatu ambazo hawakuziruhusu zingejumlisha na hiyo moja ambayo walimpa Vitus (Vitus Nkuna, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA kanda ya Nyasa) ushindi ambao hastahili, tuliposhinda tunapotaka kuanza uchaguzi upande wa wenzetu wakiongozwa na Mungai (Mwenyekiti wa zamani wa Chadema Mkoa wa Iringa, William Mungai) wakaanza kuleta fujo kutaka wajumbe wa Makete waondoke kwamba siyo halali”

Aidha Msigwa amedai kuwa kuna rushwa zilitolewa ili asishinde uchaguzi akidai kuna watu walipewa rushwa ya laki 5 mpaka milioni moja.


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

By Mujuni Henry

JUNIITV

Please disable your adblocker or whitelist this site!

         banner                            

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading