Bilionea wa Cassino wa Israel na Marekani Miriam Adelson anatarajiwa kutangaza nyongeza ya Mamilioni ya Dolla kwa kampeni ya Trump wiki hii.
Kulingana na ripoti za vyombo vya habari vya Marekani, Bi. Adelson atatoa mchango kwa kamati ya utendaji ya kisiasa iitwayo Preserve America.
Ingawa haijafahamika ni kiasi gani anapanga kutumia, katika siasa ambapo vyombo vingine vya habari vya Marekani vimeripoti kwamba mchango huo unatarajiwa kuzidi mchango wa $90m kwa Preserve America wa Bi Adelson na marehemu mumewe, Sheldon, kabla ya uchaguzi wa 2024.
Trump, Mgombea wa chama cha Republican katika uchaguzi wa Novemba wa Ikulu ya White House, alipatikana na hatia ya kughushi rekodi za biashara ili kuficha pesa zilizolipwa kwa nyota wa zamani wa filamu ya watu wazima Stormy Daniels.
Ingawa amesalia nyuma ya Joe Biden na juhudi za Democrats za kuchangisha pesa, hatia hiyo iliingiza nguvu mpya katika jitihada zake za uchaguzi huku kampeni yake ilitangazwa kwamba ilichangishwa takribani $53m (£41.6m) ndani ya saa 24 tu baada ya uamuzi huo mahakama.
Kamati za utekelezaji wa kisiasa zinaweza kutumia kiasi kisicho na kikomo cha pesa kuunga mkono wagombeaji wa nyadhifa za kuchaguliwa.
Inasamekana kuwa mabilionea wengine wana uwezekano wa kufuata mfano huo. Saa chache baada ya uamuzi huo wiki iliyopita, mabilionea kadhaa matajiri walichapisha jumbe za kumuunga mkono Trump.