MSIMU UJAO VAR ITAANZA KUTUMIKA KWA BAADHI YA VIWANJA

0:00

9 / 100

Bodi ya Ligi Kuu Bara (TPLB) imethibitisha kuwa msimu ujao utakuwa na Usaidizi wa Mwamuzi (VAR) katika Uwanja wa Benjamin Mkapa wa Jijini Dar es Salaam.

Mtendaji Mkuu wa TPLB Almas Kasongo amesema VAR itakuwepo katika uwanja huo kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

“ Msimu ujao tutakuja tofauti kidogo. Tutaboresha na tuna mpango wa kuwa nayo na CAF ndiyo wametuunga mkono na baadhi ya wataalamu wameshafika na kufunga vifaa hivyo katika Uwanja wa Mkapa.

Kasongo aliongeza kuwa uwepo wa teknolojia hiyo itakuwa sehemu ya kuwasaidia waamuzi wa Tanzania.

“ Tunaamini safari moja huanzisha nyingine, tutakuwa na katika viwanja vingine kuna partnes wetu watasaidia kwa ajili ya viwanja vingine” alisema Kasongo.

Uwepo wa VAR utakuwa nafuu ya kupunguza lawama kwa waamuzi kwa timu za Simba SC na Yanga SC ambazo zimekuwa zikiweka shinikizo kwa waamuzi katika baadhi ya michezo yao.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MAURICIO POCHETTINO AONYWA KWA KUMTUMIA VIBAYA MUDYRIK
MICHEZO Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Shakhtar Donetsk Sergei Palkin...
Read more
Alejo Veliz has completed a loan move...
Veliz, who has made eight appearances for Spurs since signing...
Read more
4 PEOPLE THAT SHOULD NOT DETERMINE YOUR...
❤ 1) Your Spiritual Fathers A Young Man came to...
Read more
DJ Cuppy’s prayer on X ignited a...
Florence Otedola, also known as DJ Cuppy, has stirred up...
Read more
LEBRON JAMES AWEKA REKODI YA KUWA MCHEZAJI...
MICHEZO Nyota wa Mpira wa Kikapu, LeBron James amevunja rekodi...
Read more
See also  Pep Guardiola says he is glad the hearing into Man City's 115 charges for alleged breaches of the Premier League's financial rules is set to begin.

Leave a Reply