ALIYEMTAPELI RIDHIWAN KIKWETE PESA AHUKUMIWA JELA MIAKA 7

0:00

10 / 100

Kijana Innocent Chengula (23) amehukumiwa kifungo cha miaka saba jela katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam baada ya kutiwa hatiani kwa makosa sita ikiwemo kujipatia kwa njia ya udanganyifu shilingi milioni nne (4) kutoka kwa Ridhiwani Kikwete ambaye ni Mbunge wa Chalinze pia Naibu Waziri Ofisi ya Rais Menejimenti na Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

Siku ya tukio Mshtakiwa huyo July 26 mwaka 2022 alijitambulisha kuwa yeye ni Katibu Mkuu Dr. Hassan Abbas na kwamba Mama yake ni mgonjwa sana hivyo anahitaji msaada wa fedha kwa ajili ya kugharamia matibabu yake ambapo kwa uungwana wake bila kusita, Naibu Waziri Ridhiwani Kikwete alimtumia pesa hiyo shilingi milioni nne.

Mbali na adhabu hiyo, pia Mahakama ya Kisutu imeitaifisha simu moja ya mkononi pamoja na laini tatu za simu alizokuwa akitumia Mshtakiwa huyo na kuwa mali ya Serikali ambapo uamuzi huo umetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Yusto Ruboroga na kuamuru pia Mshtakiwa huyo arudishe milioni nne za Naibu Waziri huyo.

Chengula ambaye ni Mkazi wa Kigogo Luhanga Jijini Dar es salaam, alikuwa anakabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na kutuma ujumbe wa maandishi kwenda katika mtandao wa kijamii wa WhatsApp ambapo alijitambulisha kwa Ridhiwani Kikwete na Rais wa TFF Wallace Karia kuwa yeye ni Dr. Hassan Abbas (Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii).

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Milan's Fonseca praises substitutes after Brugge win
MILAN, - AC Milan substitutes Noah Okafor and Samuel Chukwueze...
Read more
PAPA ASHINDWA KUJIBU SWALI KUHUSU JAMII YA...
HABARI KUU.
See also  Paul Okoye blasts Joe Igbokwe over his comment on P-Square’s split
Watu waliobadili jinsia wanaweza kuwa wazazi wa ubatizo...
Read more
SIGNS A GIRL LIKES YOU
She makes eye contact, plays with her hair, or acts...
Read more
MAKOMBORA YA ANGA YA ISRAEL YAUWA WATU...
HABARI KUU Duru za ndani nchini Israel zinasema serikali ya...
Read more
Scotland end Australia’s Grand Slam hopes with...
EDINBURGH, - Winger Duhan van der Merwe reclaimed his try...
Read more

Leave a Reply