Mabadiliko hayo katika Sekretarieti ya EAC yamefanyika baada kuondolewa kwa Peter Mathuki Machi 8, ambaye anashutumiwa katika mambo mbali mbali hasa matumizi mabaya ya madaraka.
Rais Ruto alimwita Mathuki nyumbani na kumteua kuwa Balozi wa Kenya nchini Urusi.
Mkutano huo umefanyika wakati ukanda wa Afrika Mashariki ukikabiliwa na uhaba mkubwa wa pesa.
Mwezi uliopita, Mahakama ya haki ya Afrika Mashariki (EACJ) ilitangaza kusitisha shughuli zake mwezi Juni mwaka huu baada ya kukumbwa na matatizo ya kifedha yaliyotokana na ucheleweshwaji wa kutuma pesa kutoka kwa nchi washirika wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Veronica Nduva raia wa Kenya, ameapishwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, kuchukua nafasi ya Peter Mathuki aliyeondolewa kwenye nafasi hiyo miezi kadhaa iliyopita, baada ya kuteuliwa na rais wa Kenya William Ruto kuwa Balozi nchini Urusi.
Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki chini ya Mwenyekiti wake rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, wamekutana jioni hii kwa mfumo wa video, kushuhudia upiapisho huo.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.