Narendra Modi ameapishwa kuhudumia India kwa muhula wa tatu akiwa amepata ushindi mdogo

0:00

Mwanasiasa mkongwe Narendra Modi (73), leo amekula kiapo mbele ya Rais Draupadi Murmu wa India kuwa Waziri Mkuu wa nchi hiyo kwa muhula wa tatu katika sherehe kubwa iliyofanyika Ikulu.

Katika sherehe hiyo Mawaziri wa Baraza jipya nao waliapishwa. Jiji la Delhi lilikuwa na ulinzi mkali, huku Ikulu ikizungukwa na zaidi ya askari Polisi 2,500, na hakuna Ndege iliyoruhusiwa kuruka ama kupita.

Modi ameahidi kuongoza kwa haki bila upendeleo wala ubaguzi, na amesema kuwa kipaumbele chao ni kuwawezesha masikini na watu wa tabaka la kati.

Maelfu ya wageni walihudhuria sherehe hizo wakiwemo viongozi kutokea nchi za jirani kama Bangladesh, Nepal,Sri Lanka na Maldives.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

19 INCREDIBLE THINGS THAT HAPPENS TO A...
A woman’s body unlike the man’s own is quite complicated...
Read more
WIZKID WANTED TO MARRIED CHIDINMA
CELEBRITIES CHIDINMA~~ In 2014 Wizkid reach out to me an...
Read more
Holders Manchester United visit Arsenal in FA...
Holders Manchester United will travel to record 14-times winners Arsenal...
Read more
ARSENE WENGER AISHAURI LIVERPOOL
MICHEZO Kocha wa zamani wa Arsenal, Arsene Wenger amewaonya mabosi...
Read more
TP MAZEMBE YAKANUSHA TAARIFA ZA KIFO CHA...
MICHEZO Klabu ya TP Mazembe imechapisha taarifa kuwa nguli wake...
Read more
See also  UGANDA YAJA NA MPANGO WA CCTV CAMERA KUWABAINI MAGAIDI

Leave a Reply