ZUIA MIMBA KWA NJIA YA ASILI.
Hizi ni njia za asili ambazo hutumika kupanga idadi na muda wa kupata watoto. Njia hizi hufanya kazi kwa kujichunguza na kurekodi ishara mbali mbali zinazotokea kwenye mwili wako kila siku wakati wa mzunguko wa hedhi.
Zifuatazo ni ishara zinazoonesha huenda mwanamke yuko kwenye uwezekano wa kubeba mimba.
1.siku ya 12-16 ya mzunguko wa hedhi.
- Joto la mwili kupanda.
- Kutokwa na ute mweupe mzito kwenye uke.
Kupata dalili hizi kunaweza kusaidia kujua kama kuna uwezekano wa kupata ujauzito.
Kipindi cha urutubishaji hudumu kwa siku 8-9 kwa kila mzunguko wa hedhi. Hii ni kwa sababu yai la mwanamke huishi kwa masaa 24 na mbegu za mwanaume huishi mpaka masaa 72 ndani ya mwili ya mwanamke baada ya tendo la ndoa. Hii inamaanisha kama mtafanya tendo la ndoa siku tatu nyuma kabla ya yai kuachiwa kutoka kwenye kifuko basi kuna uwezekano wa kupata ujauzito.
Ufanyaji kazi wa hizi njia za mpango hasa za asili hutegemea umri wako, Mara ngapi unashiriki tendo la ndoa na namna gani unafuata maelekezo.
Kama njia hizi za uzazi wa mpango zitatumika kulingana na maelekezo basi zina uhakika wa asilimia 99. Yaani katika wanawake mia watakao tumia njia hizi basi mwanamke mmoja tu ndio anaweza pata ujauzito. Kama hazitatumika vizuri basi wanawake wengi zaidi wanaweza kupata ujauzito.
Faida ya njia hizi za uzazi wa mpngo za asili ni kwamba hazihuzishi matumizi ya kemikali au vifaa vyovyote. Hazina madhara yoyote ya kiafya. Pia zinakubalika na imani na tamaduni zote.
Hasara za njia hizi za uzazi wa mpango ni kwamba, huchukua mizunguko 3-6 ili kujua kiuhakika kuhusu mabadiliko na ishara zinazotokea wakati wa kipindi cha kupata ujauzito, inatakiwa usifanye ngono au utumie condom wakati wa kipindi cha kupata ujauzito, pia njia hizi haziwezi kukukinga kupata magonjwa ya zinaa.
Njia za asili za uzazi wa mpango ni
- Kalenda ya mzunguko wa hedhi.
- Kumwaga mbegu za mwanaume nje ya uke.
- Kunyonyesha vizuri kipindi cha miezi sita toka kujifungua.