“KUKOPA NI AFYA KWA UCHUMI ” GEORGE SIMBACHAWENE

0

0:00

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amesema mikopo ni moja ya vyanzo vya mapato ya Serikali kote duniani, hivyo Tanzania kukopa siyo aibu wala kujidhalilisha, bali ni sifa njema kwa kuwa inakopesheka.

Simbachawene amesema hayo wakati akiongea kwenye harambee ya kuchangia fedha kwa ajili ya kubadilisha paa la Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu,Yuda Tadei Mang’ola Chini, Wilaya ya Karatu, Mkoani Arusha, ambalo limekuwa likivuja wakati wa mvua na hivyo kusababisha Wakristo kushindwa kukaa ndani.

Amesema vyanzo vya mapato vya Kanisa ni pamoja na sadaka ya kila jumapili, zaka, misaada mbalimbali pamoja na harambee huku akitaja vyanzo vya mapato vya Serikali kuwa ni kodi, tozo, misaada na mkopo, na kusema kukopa ni moja ya chanzo cha mapato ya Serikali na Serikali zote duniani zinakopa.

Amesema kama ingetokea Tanzania haiwezi kukopesheka hiyo ndo ingekuwa aibu lakini kwa kuwa inakopesheka hiyo ni heshima kubwa kwa Watanzania kwakuwa inakopa ili kutekeleza miradi ya maendeleo na kama isipofanya hivyo itapelekea Nchi kupata madhara makubwa ambayo yasingetokea kama ingekopa.

Amesema Nchi zote duniani ikiwemo Marekani na China zinakopa na zinadaiwa na kwamba kodi inayokusanywa Nchini haina uwezo wa kutekeleza miradi hiyo na kama kodi hiyo itaweza kutumika inaweza kuchukua zaidi ya miaka 40 ili kukamilisha miradi hiyo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading