MAMBO USIYOFAHAMU KUMHUSU SALLAM SK

0:00

9 / 100

Sallam Sk Ni Moja Kati Ya Nguzo Muhimu Sana Kwenye Muziki Wa Bongo Fleva Ni Mtu Ambae Akipanga Mpango Wake Huwa Haufeli, Sifa Yake Kubwa Ni Misimamo Mikali Kitu Kinachofanya Wasanii Wamuogope Sana Hata Wasanii Wa Wasafi Wanamuogopa Sana Sallam Sababu Huwa Hana Masihara Wala Urafiki Kwenye Suala La Kazi.

Watu Wengi Wamemfahamu Zaidi Baada Ya Kuanza Kufanya Kazi Na Diamond Platnumz Lakini Kabla Ya Kufanya Kazi Na Diamond Alifanya Kazi Na A.Y Na Mwana F.A Pia Alikuwa Anafanya Kazi Na Clouds Kama Agent Wa Kuleta Wasanii Wa Kigeni Kwenye Matamasha Ya Fiesta, Hivyo Msanii Yeyote Wa Kimataifa Au Kutoka Nje Ya Tanzania Uliyemuona Kwenye Fiesta Ni Kazi Ya Sallam.

Huyu Jamaa Akifanya Kazi Na Msanii Lazima Atoboe Kwenye Soko La Kimataifa, Mafanikio Ya Diamond Kimataifa Yalianzia Kwa Huyu Jamaa Baada Ya Kufanikisha Kolabo Ya Diamond Na Davido Na Kuanza Kumkutanisha Na Wasanii Wakubwa Kama NEYO, RICK ROSS, P SQUARE, Na Wengineo. Safari Ya Kwanza Ya Harmonize Kwenye Soko La Kimataifa Alipelekwa Na Sallam Ambapo Alikutanishwa Na Wasanii Wakubwa Kule Na Kutambulishwa Kama Kijana Wa Diamond Na Ikawa Rahisi Wasanii Kukubali Kufanya Nae Kazi Kwa Heshima Ya Diamond.

Kinacho Fanya Anakosa Sana Na Wasanii Ni Kwamba Wasanii Wengi Wanapenda Kupeleka Mambo Kiholela Kitu Ambacho Anaamini Kwamba Ukipeleka Mambo Kiholela Huwezi Pata Pesa Na Thamani Yako Inashuka, Huyu Jamaa Ndiye Aliyewafunza Wcb Wasafi Biashara Ya Muziki Na Hata Wasanii Waliopo Na Waliotoka Pale Wanajua Misimamo Ya Huyu Mtu Huwa Habembelezi Mtu Kabisa Haijalishi Wewe Ni Nani Sababu Kama Pesa Sallam Anayo Pesa Ya Kutosha.

See also  Why Biologically Women are More Cleverly In Relationships than Men

Anao Msemo Wake Unasema “Simsindikizi Mtu Kwenye Utajiri” Akiwa Na Maana Kwamba Kila Dili Atakalo Kamilisha Mkatie Fungu Lake Ajikatae Hata Maneno, Ndio Maana Amekuwa Akipambana Kukamilisha Madili Makubwa Ili Msanii Ukipata Pesa Nyingi Nae Atapata Nyingi Kwenye Mgao Wake. Hataki Wasanii Ambao Dili Likikamilika Wanataka Kula Peke Yao Halafu Aliye Pambana Kufanikisha Dili Anabaki Hana Kitu Anaambulia Pesa Ya Maji.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Nyumba za Mfanyabiashara na Mwanamuziki Sean ‘Diddy’...
Read more
Andrew Mlugu Amtwanga William Tai Tin Kwenye...
Tanzania leo Jumatatu Julai 29, 2024 imeanza vyema mchezo wake...
Read more
RAIS SAMIA AFICHUA UOZO WIZARA YA MAMBO...
MAGAZETI Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya leo kwenye mbao za...
Read more
SABABU YA WANAOPANGA KUZEEKA MAPEMA ...
HABARI KUU Utafiti wa chuo kikuu cha Essex cha...
Read more
SIRI WANIGERIA KUKOSA TUZO ZA GRAMMY ZA...
MICHEZO Kama kuna kitu wasanii wa Nigeria walikuwa na uhakika...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply