RAMAPHOSA AAPISHWA KUIONGOZA AFRIKA KUSINI

0:00

9 / 100

HABARI KUU

Rais Cyril Ramaphosa leo ameapishwa kwa ajili ya mhula wa pili wa urais wa kuongoza taifa la Afrika Kusini, licha ya chama chake cha African National Congress (ANC) kushindwa kupata wabunge wengi katika uchaguzi wa mwezi uliopita.

Wabunge walimchagua tena kuwa rais wiki iliyopita kufuatia makubaliano kati ya ANC na cha upinzani cha muda mrefu cha Democratic Alliance (DA) pamoja na vyama vingine na hivyo kuunda serikali ya mseto.

Chama cha ANC, ambacho kimetawala tangu kumalizika kwa ubaguzi wa rangi mwaka 1994, kilipoteza wingi wa viti vya ubunge kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 30 na hivyo kutotoa mshindi wa moja kwa moja.

Viongozi kutoka mataifa mbalimbali akiwemo Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania wamehudhuria hafla hiyo.

“Ninaapa kwamba nitakuwa mwaminifu kwa Jamhuri ya Afrika Kusini. Nitatii, nitazingatia katiba na sheria nyingine zote za jamhuri,” ameapa Ramaphosa mbele ya Jaji Mkuu Raymond Zondo.

Chama cha uMkhonto weSizwe (MK) kilichoundwa miezi sita iliyopita na Rais wa zamani wa nchi hiyo, Jacob Zuma kimesusa kikisema hakiwezi kushiriki katika uapisho huo wa “kifahari”.

Chama hicho ambacho kilipata asilimia 15 ya kura na viti 58 vya ubunge, pia kilisusia kikao cha kwanza cha Bunge Ijumaa iliyopita.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

KWANINI MAANDAMANO YA KENYA YANAMG'OA IGP KOOME?
HABARI KUU Viongozi wa muungano wa upinzani wa Azimio siku...
Read more
ANTONIO CONTE KWENYE RADA ZA FC BAYERN...
MICHEZO Miamba ya soka nchini Ujerumani FC Bayern Munich imeripotiwa...
Read more
Peter Obi criticizes Tinubu's administration for proposing...
POLITICS
See also  How Davido has sacked his long-time friend and lawyer Bobo Ajudua
Presidential candidate Peter Obi of the Labour Party has...
Read more
MANCHESTER UNITED YANASA MTAMBO WA MABAO
MICHEZO Manchester United wameulizia upatikanaji wa Mshambuliaji wa Stuttgart. Sehrou...
Read more
ANTHONY MARTIAL KUONDOKA MANCHESTER UNITED
MICHEZO Mshambuliaji wa Man Utd, Anthony Martial ataondoka kwenye kikosi...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply