KWANINI MAHUJAJI WANAKUFA KWENYE MIJI YA MAKKAH NA MADINA?

0:00

9 / 100

HABARI KUU

Mamia ya mahujaji wamefariki dunia na maelfu wanatibiwa kutokana na magonjwa yanayotokana na joto kali walipokuwa wanatekeleza ibada ya kila mwaka ya Hija mjini Makkah, Saudi Arabia, huku joto likifikia nyuzi 49 (Fahrenheit 120).

Wakati CNN ikisema waliokufa ni mamia, India Today imetaja zaidi ya 1,000 na The Guardian la Uingereza limetaja watu 550.

Kwa mujibu wa CNN, Waindonesia 165 ni miongoni mwa mahujaji waliofariki dunia, Wajordan 41, Watunisia 35 na Wairani 11.

Taarifa ya CNN inasema raia wengine 22 wa Jordan hawajulikani walipo na Wairani 26 wamelazwa hospitalini.

Chanzo: Mashirika mbalimbali ya habari

India Today imesema miongoni mwa waliokufa ni Wamisri 650. Mpaka sasa hakuna taarifa yoyote ya Watanzania kuhusiana balaa hilo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Lopez urges Girona to keep fighting...
David Lopez scored Girona’s first ever Champions League goal but...
Read more
AZIZ KI AWEKA REKODI MPYA LIGI KUU...
MICHEZO Kiungo Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young...
Read more
MPINZANI NCHINI CHAD ATEULIWA KUWA WAZIRI MKUU...
HABARI KUU. Rais wa mpito nchini Chad 🇹🇩, Mahamat...
Read more
Peter Okoye reacts over Paul’s song theft...
Peter Okoye, the renowned musician, has responded to the allegations...
Read more
Victor Olatunji scores on his first Champions...
Sparta Prague made a strong return to the Champions League...
Read more
See also  SERIKALI YAWAITA WAWEKEZAJI KWENYE SGR

Leave a Reply