Imegundulika kwamba sokwe hula miti ambayo ina uwezo wa kutuliza maumivu na kuzuia bakteria wanapoumwa, wanasayansi wamegundua.
Watafiti wamegundua hilo wakati wanafanya kazi ya uchunguzi katika msitu mmoja nchini Uganda ambako utafiti wao ulilenga kuangalia sokwe waliojeruhiwa au kuugua ili kujua iwapo walikuwa wanajitibu kwa mimea au la.
Wakati mnyama aliyejeruhiwa alipotafuta kitu maalumu kutoka kwenye mimea ili kula, watafiti walikusanya sampuli za mmea huo na wakafanya vipimo. Mimea mingi iliyopimwa imeonekana kuwa na nguvu za kupambana na bakteria.
Wanasayansi, ambao wamechapisha matokeo yao katika jarida la PLOS One, wanafikiri sokwe wanaweza kumsaidia mwanadamu katika kutafuta dawa mpya zinazotokana na miti.
“Hatuwezi kupima kila kitu katika misitu hii kwa sifa zake za dawa, mtafiti mkuu Dkt. Elodie Freymann, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford, amesema. “Kwa hivyo kwa nini tusifanyie vipimo mimea ambayo tuna habari hii – mimea ambayo sokwe wanaitafuta (wanapoumwa au kujeruhiwa)?”
Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, Dkt. Freymann ametumia miezi kadhaa kufuata na kutazama kwa makini jamii mbili za sokwe katika Hifadhi ya Msitu Mkuu wa Budongo.
Pamoja na kutafuta dalili za maumivu – mnyama akichechemea au kuushika mwili wake kwa njia isiyo ya kawaida – yeye na wenzake walikusanya sampuli za kinyesi na mkojo ili kuangalia ugonjwa na maambukizi.
Walizidisha umakinifu wao wakati sokwe aliyejeruhiwa au mgonjwa alipotafuta kitu ambacho kwa kawaida huwa hawali – kama vile magome ya mti au maganda yama matunda.
“Tulikuwa tunatafuta dalili hizi za kitabia kwamba mimea inaweza kuwa dawa,” Dk Freymann ameelezea.
Kwa jumla, watafiti walikusanya sampuli 17 kutoka kwa aina 13 tofauti za mimea na kuzipeleka kufanyiwa majaribio na Dk Fabien Schultz, katika Chuo Kikuu cha Neubrandenburg cha Sayansi nchini Ujerumani.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.