WANAODAIWA KUJIHUSISHA NA BIASHARA YA UKAHABA KULIPWA MABILIONI

0:00

10 / 100

HABARI KUU

Mkuu wa Wilaya ya Ubungo (DC) Hassan Bomboko ametakiwa kulipa kiasi cha Sh. Bil 36 kutokana na sakata la ukamataji wanawake 36, wanaodaiwa kujihusisha na biashara ya ukahaba.

Suala hilo limechukua sura mpya, baada ya DC huyo kupewa notisi ya kuwalipa kiasi hicho wanawake hao.

Notisi hiyo ya wiki mbili imeanza jana Alhamisi, Juni 20, 2024 na inalenga kuwalipa watuhumiwa hao 36 wanaodai kudhalilishwa kwa kuwaita ‘Dada Poa’ na kuwaweka rumande kwa siku tano kinyume na sheria.

Notisi hiyo imeandikwa na wakili wao kutoka tasisi ya Stalwart, Peter Madeleka ambaye amethibitisha kwamba tayari wameshaiwasilisha kwa kiongozi huyo.

DC Bomboko alisema alikuwa hajapokea notisi hiyo inayoelezwa amepelekewa. ” Sijapokea hiyo notisi. Muulizeni vizuri.” Alipotafutwa tena jioni hakupatikana.

Hivi karibuni iliwakamata ‘makahaba’ hao Ubungo, River Side na Sinza, bado inavuta hisia za wengi mitandaoni wakieleza inaingilia faragha za watu na inakiuka haki za binadamu.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Licha ya msimu ujao Simba sc ...
Mashindano ya CAF msimu wa 2024/25 yataanza kwa raundi ya...
Read more
LIGI KUU ENGLAND YA MOTO ...
Michezo Mwendelezo wa Ligi kuu ya England umeendelea hivi leo...
Read more
FAIDA ZA KULA NDIZI MBIVU KWA MWILI...
AFYA FAIDA ZA NDIZI MBIVU Ndizi ina aina tatu za...
Read more
AIPONGEZA MAHAKAMA KWA KUHUKUMIWA KIFUNGO CHA MAISHA...
Mfanyabiashara aliyekuwa akimiliki kiwanda bunu cha kutengeneza na kusambaza pombe...
Read more
FASTEST WAY TO DESTROY YOUR LIFE ...
OUR STAR 🌟
See also  JINSI BWAWA LA NYERERE LILIVYOJENGWA KISAYANSI
"Fastest way to destroy your life" -...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply