“Kama Wanauza Miili Yao Wao Wanabaki na Nini?”

0:00

9 / 100

Shahidi wa pili katika kesi ya ukahaba inayowakabili washtakiwa watano katika mahakama ya Hakimu mkazi Sokoine Drive, ameieleza mahakama hiyo kuwa waliwakamata washtakiwa hao kwa tuhuma za ukahaba kutokana na viashiria vya aina ya mavazi waliyokuwa wameyavaa na muda na waliokutwa na polisi.

Hata hivyo, Shahidi huyo ambaye ni askari kutoka Kituo cha Polisi Mburahati, WP Konstebo wa Polisi (PC), Tunusuru Malingula alijikuta katika wakati mgumu alipotakiwa kueleza maana ya ‘Umalaya’ au ‘Ukahaba’ kutokana na viashiria hivyo alivyotaja.

Ilikuwa ni wakati wa maswali ya dodoso aliyoulizwa na mawakili wa utetezi katika kesi hiyo, Peter Madeleka, Jebra Kambole na Maria Mushi, leo alhamisi Juni 27,2024 na akajibu kuwa hajui maana ya ukahaba.

Pia, amesema hajui kama kuna sheria inayobainisha sifa za mavazi yanayoashiria ukahaba wala inayoweka muda ambao mtu akikutwa barabarani anakuwa anajihusisha na ukahaba.

Shahidi huyo pia alitakiwa kueleza kama washtakiwa walikuwa miili yao, wao walibaki na nini na wateja walionunua wako wapi.

Washtakiwa katika kesi hiyi inayosikilizwa na Hakimu Mfawidhi Rachel Kasebele ni Mariam Yusuph (25) mkazi wa magomeni, Mwazani Nassoro (25) mkazi wa kigogo, Mwanaidi Salum (25) Mkazi wa Mabibo, Faudhia Hassan (35) mkazi wa Ubungo na Tatu Omary (40) Mkazi wa Ubungo.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

EMILIO NSUE LOPEZ AMETANGAZA KUSTAAFU SOKA ...
MICHEZO NAHODHA wa Timu ya Taifa ya Guinea ya Ikweta,...
Read more
WAUMINI WALALAMIKA KUNYANYASWA KINGONO KANISA LA TB...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
Rais Samia agawa zawadi ya Tausi
HABARI KUU
See also  President Ruto Appoints New Leaders to Key Government Positions
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amemzawadia Rais...
Read more
RAIS SAMIA SULUHU ZIARANI KOREA KUSINI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia...
Read more
WAFAHAMU WAAMUZI WA YANGA NA AL AHLY
MICHEZO Mechi kati ya Al Ahly na Young Africans itachezeshwa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply