Aina za UTI SUGU kwa Mwanamke na Mwanaume

0:00

11 / 100

U.T.I ni nini?

U.T.I(Urinary Tract Infection) kwa wanawake ni maambukizi ya mfumo wa mkojo kwa wanawake ambao huhusisha figo (kidney), kibofu cha mkojo (urinary bladder), mrija wa mkojo kutoka kwenye kibofu cha mkojo (urethra) pamoja na mrija unao unganisha figo na kibofu cha mkojo (ureter).

Maambukizi haya kwa kiasi kikubwa husababishwa na bakteria jamii ya E. coli, lakini katika mazingira machache fangasi na virusi wanaweza kuwa chanzo cha maambukizi haya.

Aina Za UTI Kwa Wanawake.

Zifuatazo ni aina mbili za u.t.i kwa wanawake ambazo ni;

  1. Lower U.T.I.
    Hii ni hatua ya ugonjwa kushambulia maeneo ya urethra na kibofu cha mkojo ambapo katika hatua hii, mgonjwa atakuwa na dalili zifuatazo:Maumivu wakati wa kukojoa, kujiskia kukojoa mara kwa mara lakini kutoa mkojo kidogo tu (polyuria), damu katika mkojo (hematuria), maumivu ya kiuno kwa wanawake, kukojoa mkojo wenye harufu kali.
  2. Upper U.T.I.
    Haya ni maambukizi ya ndani ya figo.Hii ni hatua mbaya sana endapo bakteria wataanza kuingia kwenye mfumo wa damu kutoka kwenye figo (sepsis). Sepsis huweza kusababisha msukumo wa damu kuwa mdogo sana (low blood pressure), mshituko au kifo. Katika hatua hii, mgonjwa atakuwa na dalili zifuatazo: Maumivu ya maeneo juu ya mgongo, homa, kutapika, kichefuchefu.

Chanzo Cha U.t.i Kwa Wanawake:

U.t.i husababishwa na bakteria waitwao Escherichia coli (E.coli), bakteria hawa wanapoingia mwilini huenda kuathiri mfumo wa mkojo.
Mambo yafuatayo yanaweza kumuweka mwanamke kwenye hatari ya kupata U.t.i;

  1. Kinga ya mwili kutokuwa imara (immunosuppresion).
  2. Kutumia vifaa au dawa za kuzuia mimba.
  3. Kupungua kwa homoni ya estrogen.
  4. Ugonjwa wa kisukari.
  5. Kutumia choo kichafu.
  6. Kufanya ngono isiyo salama (unprotected sexual intercourse).
    Mimba (Pregnancy).
See also  JOSE MOURINHO AMPA ONYO MIKEL ARTETA

Sababu Za U.t.i Kwa Mwanamke:

Mwanamake huwa na uwezekano mkubwa zaidi wa kuugua ugonjwa huu pamoja na kujirudia mara kwa mara kwa kuwa mrija wa mkojo huwa ni mfupi sana tofauti na mwanaume, pia tundu la uke huwa karibu na sehemu ya haja kubwa hivyo ni rahisi kwa bakteria kutoka kwenye choo kuingia ukeni.

Pia, matumizi ya baadhi ya njia za uzazi wa mpango, kemikali kali kusafishia via vya uzazi, kufikia umri wa ukomo wa hedhi pamoja na ujauzito ambao hubana kibofu cha mkojo na kupunguza ufanisi wake kwenye kutoa mkojo wote huwa ni baadhi ya sababu zinazoongeza uwezekano wa mwanamke kuugua ugonjwa huu kuliko mwanaume.

Dalili za U.T.I

Dalili za uti zinaweza kutofautiana kulingana na sehemu ya mfumo wa mkojo ilioathiriwa (kama vile kibofu cha mkojo, urethra, au figo) na kwa kiwango cha maambukizi.
Zifuatazo ni dalili za kawaida za uti ambazo ni pamoja na:

1) Kukojoa Mara Kwa Mara.

Moja ya dalili za kawaida za uti ni haja ya kukojoa mara kwa mara.
Hii inaweza kuambatana na hisia ya kuchoma au kuwaka wakati wa kukojoa.

2) Maumivu Kwenye Sehemu Ya Chini Ya Tumbo.

Unaweza kuhisi maumivu au joto kwenye eneo la chini la tumbo, haswa karibu na mfupa wa nyonga.

3) Haja Ya Kukojoa Mara Kwa Mara Usiku.

 Watu wenye uti mara nyingi wanahisi haja ya kukojoa usiku hali inayojulikana kwa kitaalam kama Nocturia, ambayo inaweza kuvuruga usingizi wao.

4) Kukojoa Kidogo Kwa Kila Wakati.

Wakati mwingine, unaweza kuhisi kama unahitaji kukojoa sana, lakini unapokwenda kwenye choo, unatoa kiasi kidogo cha mkojo.

See also  MADHARA YA FANGASI UKENI NA TIBA YAKE

5) Mkojo Mweusi Au Una Harufu Mbaya.

Mkojo unaweza kubadilika rangi kuwa giza au una harufu mbaya kutokana na uwepo wa maambukizi.

6) Maumivu  Ya Chini Ya Mgongo. 

Kwa baadhi ya watu, uti unaweza kusababisha maumivu ya chini ya mgongo au upande wa chini wa mwili kama ishara ya maambukizi ya figo.

7) Kichefuchefu Na Kutapika.

Baadhi ya watu wanaweza kuwa na kichefuchefu au kutapika kama matokeo ya uti, haswa ikiwa maambukizi yamefika kwenye figo.

8) Kuhisi Udhaifu Au Uchovu.
Uti inaweza kusababisha hisia za udhaifu au uchovu.

Madhara ya UTI SUGU

Kama UTI haipatiwi matibabu ipasavyo, inaweza kusababisha madhara makubwa kwa mwili, ikiwa ni pamoja na:

  1. Kupanda kwa maambukizi kwenye figo – UTI sugu inaweza kusababisha maambukizi kupanda kutoka kwenye kibofu cha mkojo hadi kwenye figo, hali inayojulikana kama pyelonephritis. Hii inaweza kusababisha dalili kali kama vile homa, maumivu makali ya mgongo na kichefuchefu.
  2. Kupungua kwa kiwango cha kufyonza maji mwilini – UTI sugu inaweza kusababisha kibofu cha mkojo kushindwa kufanya kazi vizuri na hivyo kupunguza kiwango cha kufyonza maji mwilini. Hii inaweza kusababisha kuongezeka kwa kiu, ukavu wa kinywa, na kushuka kwa shinikizo la damu.
  3. Kuongezeka kwa hatari ya kupata magonjwa mengine – UTI sugu inaweza kusababisha mfumo wa kinga kuwa dhaifu na hivyo kuongeza hatari ya kupata magonjwa mengine kama vile maambukizi ya njia ya mkojo na ugonjwa wa figo.
  4. Kuathiri uwezo wa kushika mimba – UTI sugu inaweza kusababisha uharibifu kwenye mfumo wa uzazi kwa wanawake na hivyo kupunguza uwezo wao wa kushika mimba.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

See also  CHELSEA KUMPA MKATABA MPYA COLE PALMER

Related Posts 📫

$220m Fine: FCCPC replies WhatsApp over Nigeria...
The Federal Competition and Consumer Protection Commission has described Meta’s...
Read more
Musician Davido expresses joy as his uncle,...
Famous Nigerian Afrobeat musician David Adeleke, whose stage name is...
Read more
MJAMZITO WA MAPACHA WA MIEZI NANE ACHINJWA...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
MESSI KUWEKA REKODI HII MPYA ...
MICHEZO Nyota wa soka Lionel Andres Messi huenda akaongeza rekodi...
Read more
MAMBO YA KUZINGATIA KIJANA UNAPOTAKA KUOA.
Leo sina maneno mengi. Kijana Sasa umekuwa Mkubwa, imefikia hatua...
Read more

Leave a Reply