Kwanini Mahakama imemfutia Donald Trump mashitaka yanayomkabili?

0:00

12 / 100

WASHINGTON

Mahakama Kuu ya Marekani imeamua kwamba Donald Trump hawezi kushtakiwa kwa matendo ambayo yalikuwa ndani ya mamlaka yake ya kikatiba kama Rais katika uamuzi wa kihistoria unaotambua kwa mara ya kwanza aina yoyote ya kinga ya Rais dhidi ya mashtaka.

Majaji, katika uamuzi wa 6-3 ulioidhiishwa na Jaji Mkuu John Roberts, wametupilia mbali uamuzi wa mahakama ya chini ambao ulikuwa umekataa madai ya Trump ya kinga dhid ya mashtaka ya jinai ya shirikisho yanayohusiana na juhudi zake za kubatilisha kushindwa kwake na Rais Joe Biden katika uchaguzi wa 2020.

Majaji sita wasiopenda mabadiliko wameunga mkono uamuzi huo wa Mahakama Kuu, wakati watatu wa mrengo wa kushoto wamepinga.

“Tumehitimisha kwamba chini ya muundo wetu wa kikatiba wa kugawanya madaraka, asili ya mamlaka ya Rais inataka kwamba Rais wa zamani awe na kinga fulani dhidi ya mashtaka ya jinai kwa matendo rasmi wakati wa kipindi chake ofisini,” amesema Jaji Roberts.

Trump ni mgombea wa Chama cha Republican anayemkabili mgombea wa Democrat Rais Biden katika uchaguzi Mkuu wa Marekani Novemba 5, 2024 katika marudio ya uchaguzi wa 2020.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

19 ROMANTIC THINGS TO DO THAT DON'T...
When romance is often mentioned, many think it is all...
Read more
Israel ilivyohusika kwenye kifo cha Rais wa...
HABARI KUU Rais wa Iran Ibrahim Raisi (63), Waziri wa...
Read more
COMMON MONEY MISTAKES TO AVOID
BUSINESS 10 common money mistakes to avoid Mistake 1 Not...
Read more
CASEMIRO KWENYE RADA ZA WAARABU ...
MICHEZO
See also  WATU 9 WAFARIKI BAADA YA GARI LAO KUSOMBWA NA MAJI
Manchester united ipo tayari kumpiga bei nyota wake wa...
Read more
VITA YA URUSI NA UKRAINE YAMUONDOA KIONGOZI...
HABARI KUU. Kevin Mccarthy anakuwa spika wa kwanza wa Bunge...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply