Waingereza wapiga kura Labour ikitabiriwa kushinda

0:00

10 / 100

Wananchi wa Uingereza wanaendelea kupiga kura katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kukirejesha madarakani chama kikuu cha upinzani cha Labour, na kumaliza takribani muongo mmoja na nusu wa utawala wa chama cha Conservative.

Huu ni uchaguzi wa kwanza wa kitaifa tangu Boris Johnson aliposhinda kwa kishindo kura ya mwaka 2019. Unafanyika baada ya Waziri Mkuu Rishi Sunak kuchukua hatua ya kushangaza ya kuitisha uchaguzi huo miezi sita mapema kuliko ilivyotakiwa.

Upigaji kura ulianza tangu saa moja kamili asubuhi kwa saa za Uingereza kwenye zaidi ya vituo 40,000 vya kupigia kura nchini kote.

Rishi Sunak alikuwa miongoni mwa watu wa kwanza waliojitokeza kupiga kura katika jimbo lake la Richmond na Northallerton huko Yorkshire, kaskazini mwa England, akiwa ameongozana na mkewe Akshata Murty.

Baada ya miaka 14 madarakani chini ya mawaziri wakuu watano ndani ya kipindi cha miaka minane, chama cha Sunak cha Conservative kinatarajiwa kushindwa na chama cha Labour kinachoongozwa na Keir Starmer, chenye kufuata siasa za mrengo wa kushoto.

Starmer amepiga kura katika jimbo la Holborn na St. Pancras, kaskazini ya London, akiwa ameongozana na mkewe Victoria. Chama cha Sunak kimekuwa kikijitahidi kuwahakikishia wapiga kura kuhusu masuala kama vile kupanda kwa gharama ya maisha na mzozo katika Huduma ya Taifa ya Afya.

Kama chama Labour kitashinda, Uingereza itarudi kwenye mrengo wa wastani wa kushoto baada ya karibu muongo mmoja na nusu wa serikali za mrengo wa kulia za chama cha Conservative.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MSANII WA VICHEKESHO SMOTHER AFARIKI ...
NYOTA WETU
See also  GIORGIA MELONI AOMBA KULIPWA FIDIA KWA KUHUSISHWA NA VIDEO ZA NGONO
Msanii nguli wa vichekesho, Tom Smothers ambaye ni...
Read more
Rekodi ya Pep Guardiola dhidi ya Alex...
MICHEZO Baada ya kuiongoza Manchester City kushinda ubingwa wa Ligi...
Read more
HIZI NDIZO FAIDA ZA ULAJI WA BAMIA
MAKALA Wataalam wa Tiba Mbadala, wanaarifu kwamba ukichukua Bamia na...
Read more
Minister of Women Affairs has initiated legal...
HARD NEWS Minister of Women Affairs has initiated legal action against...
Read more
UMEME WAMPASUA KICHWA NAIBU WAZIRI MKUU ...
Magazeti Karibu Mtanzania kwenye magazeti ya hivi leo, yakiwa na...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply