Ugonjwa wa Tezi Dume: Chanzo,Dalili na Tiba yake

0

0:00

AFYA YA TEZI DUME KWA MWANAUME

Kila mwanaume anazaliwa na Tezi ya kiume.

Tezi dume siyo ugonjwa bali ni moja ya tezi kama tezi nyingine mwilini.

Tezi dume inapatikana katika mfumo wa uzazi wa mwanaume katika shingo ya kibofu cha mkojo.

Kazi yake kubwa nikutengeneza majimaji ya uzazi wa mwanaume (shahawa), ambayo husaidia kurutubisha mbegu za kiume zilizo tengenezwa kutoka kwenye Korodani na hivyo mbegu za kiume kubaki hai kwa muda mrefu na unaostahili.

Tatizo linakuja kiungo hiki kinapoanza kutanuka. Kiungo hiki kinatanuka taratibu taratibu na kasi ya utanukaji wake hutofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine.

Hili ni tatizo linalo wakumba wanaume wengi kwa sasa.

Takwimu zinaonesha kwamba kati ya wanaume 10, wa 3 na kuendelea wana dalili za kutanuka kwa Tezi dume.

NINI MAANA YA UKUAJI WA TEZI DUME?

Ukuwaji wa Tezi dume ni ile hali ya chembe chembe hai katika tezi ya kiume kukua bila kufuata utaratibu wa mfumo wa mwili katika eneo linalo zunguka mirija ya kupitisha mkojo na mbegu za kiume.

Tatizo hili kwa sasa linawapata wanaume kuanzia umri wa miaka 25 na kuendelea, tofauti na awali lilikuwa likijitokeza kuanzia miaka zaidi ya 50.

Takwimu kutoka kwenye shirika la CHRP (Centre for Human Right Promotion), zinaonesha kwamba kiujumla kila mwanaume katika maisha yake ana 16% za kugundulika na saratani ya Tezi Dume, na

mtu 1 kati ya watu 6 analo hili tatizo; 3% (1 kati 33) wanakufa kwasababu ya Saratani ya Tezi Dume.

Saratani hii inaua mwanaume mmoja kila baada ya dakika 13.

II. VYANZO VINAVYOPELEKEA TEZI DUME KUTANUKA

Tatizo la kutanuka kwa tezi dume limekuwa kwa kasi sana hii ni kutokana na mitindo ya maisha wanaume wengi wanayoishi hasa katika kipindi hiki cha sasa.

Pia na elimu ndogo iliyoko kwenye jamii kuhusu afya zao.

Vifuatavyo ni vyanzo vinavyoweza kupelekea kutanuka kwa tezi dume

  • Ukosefu wa lishe kamili na Virutubisho muhimu mwilini
  • Uwepo wa sumu nyingi mwilini
  • Kutokufanya mazoezi
  • Matumizi ya pombe kali, na uvutaji wa sigara
  • Uzito mkubwa (uliopindukia, uliokithiri), na Kitambi
  • Kutokukaa sawa kwa vichocheo vya mwili (Hormone Imbalance)
  • Msongo wa mawazo ( Stress )
  • Magonjwa ya zinaa
  • Umri mkubwa
  • Upasuwaji wa korodani, kuzaliwa na korodani moja,
  • Historia ya Familia (Kurithi)
  • Sababu za kimazingira (Ethnicity)
See also  FAIDA ZA KULA NDIZI MBIVU KWA MWILI WA MWANAMKE

III. DALILI ZA KUTANUKA KWA TEZI DUME

Mtu mwenye tatizo katika tezi huanza kwa dalili ndogo ndogo sana,

Mpaka mtu apate saratani ya Tezi Dume (Prostate Cancer), ujue amekaa na tatizo hilo kwa muda mrefu, si chini ya miaka isiyopungua 10.

Hii hutokana na mrundikano wa mkojo unaobaki kwenye kibofu na kwenye mrija wa mkojo (Urethra) wakati unakojoa; ukiendelea kujirundika kwenye kibofu na mrija; baada ya muda unazalisha “Uric Acid” na ndio inatengeneza saratani (cancer).

Saratani ziko katika hatua nne.

Ya kwanza na yapili ukiwahi unaweza kupona; lakini ikishafika stage ya 3 na 4, hazitibiki bali Unasaidiwa kupunguza makali kwa mionzi ukijitayarisha kupoteza maisha muda wowote.

Hivyo ukiona dalili mojawapo kati ya hizi chukua tahadhari na hatua mapema kabla hujaharibu mfumo wako

mzima wa uzazi wa mwanaume.

a) Dalili za awali

  • Kukojoa mkojo uliochanganyikana na damu
  • Kukojoa mkojo wenye mtiririko dhaifu
  • Maumivu kwenye mfumo wa mkojo
  • Kuhisi maumivu wakati wa kukojoa
  • Kuhisi kibofu kimeja mkojo muda wote na ukienda kukojoa mkojo hautoki, lakini ukirudi kukaa unahisi kukojoa tena.
  • Homa
  • Kukojoa mara kwa mara wakati wa usiku

b) Dalili za mtu aliyeathirika

  • Maumivu ya mifupa hasa chini ya mgongo, kiuno na mbavu
  • Miguu kuwa dhaifu
  • Kushindwa kumudu tendo la ndoa , au Kuhisi maumivu makali wakati unamaliza tendo la ndoa
  • Kushindwa kuzuia mkojo, pindi unapohisi kukojoa
  • Kushindwa kuzuia haja kubwa (kinyesi cha maji maji)
  • Tumbo kuja gesi mara kwa mara

IV. MADHARA YA TEZI ILIYOTANUKA

Katika hatua za awali, tezi inapotanuka hugunduliwa kwa kupimwa kwa njia ya kidole. Hii ni njia ambayo daktari huingiza kidole kwenye njia ya haja kubwa ili kuweza kubaini kama tezi imetanuka. Kipimo hiki ndicho rahisi kinacho kubalika duniani kote na kisicho na gharama.

Lakini kimekuwa kikipata upinzani kutoka kwa wanaume kutokana na imani potofu ya wahusika wa tatizo hili kuona ni udhalilishaji.

Kipimo kingine ni kipimo cha damu. Damu huchunguzwa aina ya protein inayozailishwa na seli za tezi dume, kiitwacho Prostate Antigen (PSA). PSA huonesha kuwapo kwa tatizo kwenye Tezi Dume, lakini kipimo hiki hakina uwezo wa kutofautisha endapo tatizo hilo linamaanisha saratani.

See also  Sababu za Kujifungua Mtoto Mwenye Uzito Pungufu

Yafuatayo ni madhara ya tezi iliyotanuka

  • Kibofu cha mkojo kuuma: hivyo hupelekea mkojo kurudi juu, na kuharibu figo na Ini n.k.
  • Kufunga kwa njia ya mkojo kabisa
  • Figo kushindwa kufanya kazi (Kidney Failure)
  • Kushindwa kumudu tendo la ndoa (Ndoa zinavunjika)
  • Ugumba (Infertility, Frigidity for men)
  • Kutokea kwa majipu sehemu ya Tezi Dume
  • Kifo

V. SULUHISHO KWA TEZI ILIYOTANUKA

SULUHISHO PENDWA

a) Suluhisho Linalopendwa

Watu wengi hukimbilia hospitali pindi wanapopatwa na madhara ya Tezi dume na kujikuta wakipewa tiba ambazo huficha tatizo hilo kwa muda mfupi kisha tatizo hujirudia kwa kasi kubwa.

Tezi iliyotanuka haiwezi kutibika kwa njia za madawa yenye makemikali au mitishamba, lakini madawa au upasuaji hupunguza maumivu ya dalili na kuzifanya zisizidi sana.

Kuna njia 3 za kudhibiti Tezi iliyotanuka

  1. Kusubiri na kufuatilia kwa ukaribu na Daktari:

Inashauriwa kwamba kwa tatizo hili ni bora kuendelea kulichunguza bila kukimbilia tiba kali kama madawa, upasuaji na Tiba kemikali, mpaka pale mtu atakapoona hakuna njia mbadala.

  1. Madawa

“Baadhi ya madawa wanayopewa wagonjwa wa saratani ya tezi Dume yaligunduliwa miaka 30 iliyopita, yanasababisha athari kwenye Ini, Moyo na kuvimbisha magoti. Yamepigwa marufuku katika Nchi haswa za Ulaya.”

– Johnathon Waxman, Cancer Specialist, Hammer Smith Hospital, London

  1. Upasuaji

Njia hii ambayo madaktari hutumia inapelekea “70% ya wagonjwa kuwa mahanithi baada ya upasuaji, na 40% wanashindwa kuzuia mkojo kutoka wanapo banwa na haja ndogo.”

– Johnathon Waxman

Inasikitisha kuona wanaume wanapasuliwa bila uhakika wowote kwamba huo upasuaji utakuwa na manufaa.

SULUHUSHO LA KUDUMU

b) Suluhisho la Virutubisho (Supplements)

Tafiti zinaonesha kuwa kutanuka kwa Tezi dume kwa asilimia kubwa zaidi husababishwa na upungufu wa madini na virutubisho ambavyo mwili unavihitaji ili kuweza kuboresha afya ya Tezi na uzazi.

Upungufu huu hupelekea kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa kasi ya kutanuka kwa tezi na hatimaye Kansa ya Tezi dume.

Hivyo basi program maalumu ya virutubisho(Supplements) imeandaliwa

See also  Aina za UTI SUGU kwa Mwanamke na Mwanaume

Kwa watu wenye changamoto hii na pia kwa watu wanaohitaji kuboresha na kuongeza vitamins,Madini ambayo huondoa athari na dalili za kutanuka kwa Tezi Dume, na mfumo wa uzazi mwanaume(Nguvu za kiume).

Virutubisho hivi sio dawa wala mitishamba.

Zimetengenezwa kutoka kwenye organic materials au vyakula ambavyo tungefaa kula kila siku, na vina lishe kamili na virutubisho muhimu katika mwili wa mwanaume ili kutengeneza afya bora na nadhifu.

Virutubisho hivi vina mchanganyiko wa vitu vifuavyo: Proteins, Vitamins, Minerals, Essential Fat Acid and Trace minerals.

Kwa pamoja husaidia katika:

  • Kuimarisha kinga ya mwili dhidi ya Bacteria na virus ambao huweza kupelekea cancer ya tezu dume.
  • Husaidia katika kuweka sawa kiwango cha sukari mwilini, kama vile uwepo wa SELENIUM katika virutubisho hivi husaidia katika kuboresha utendaji kazi wa insulini mwilini. Hivyo kuthibiti kiwango cha sukari na sumu mwilini.
  • Husaidia katika kuondoa Cholesterol mbaya mwilini na hivyo kufungua mirija ya kibofu na hivyo kupata haja ndogo vizuri.

— Husaidia katika kuongeza uzalishaji wa mbegu za kiume na kuboresha utendaji kazi wa mirija ya Tezi na hivyo kuimarisha utendaji kazi wa tezi.

  • Huondoa maumivu, na kuongeza nguvu.
  • Husaidia katika kuupa mwili nguvu, kuongeza uzalishaji tishu katika mwili

Kuboresha mzunguko wa damu, vitamins na madini

Na kuongeza kiwangi cho uzalishaji mbegu kwa mwanaume.

Matumizi bora ya Virutubisho ni muhimu sana katika kuboresha Afya ya uzazi kwa mwanaume na kuondoa athari za Tezi Dume.

Kwa yeyote mwenye tatixo la tezi dume na anayehitaji kupata virutubisho hivi kwaajili ya kuboresha na kuimarisha afya yake ya Tezi Dume (Prostate Gland) na mfumo mzima wa uzazi wa mwanaume.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV


Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Don't miss out!
Invalid email address

Leave a Reply

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe now to keep reading and get access to the full archive.

Continue reading