Uhispania imetinga fainali ya kombe la Mataifa Ulaya EURO 2024 kufuatia ushindi wa 2-1 dhidi ya Ufaransa katika dimba la Allianz Arena na kuisukumiza Ufaransa nje ya michuano hiyo.
Bao la kichwa la Randal Kolo Miami liliipatia Ufaransa bao la uongozi la mapema mnamo dakika ya 8 huku goli maridadi la Lamine Yamal kuisawazishia Uhispania kabla ya Dani Olmo kufunga bao la uongozi na la ushindi kwa Mabingwa hao mara tatu ya EURO.
Lamine Yamal akiwa na umri wa miaka 16 na siku 362 amekuwa mchezaji kinda zaidi kufunga bao kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano akiipiku rekodi ya Johan Vonlanthen miaka 18 na siku 141 ambaye pia alifunga bao dhidi ya Ufaransa kwenye EURO 2004.
FT: Uhispania 🇪🇸 2-1 🇫🇷 Ufaransa
⚽ Yamal 21’
⚽ Olmo 25’
⚽ Kolo 8’
Uhispania imetangulia fainali kumsubiri mmoja kati ya England au Uholanzi kwenye nusu fainali ya pili kesho.
HIZI HAPA TAKWIMU ZA LAMINE YAMAL KIJANA MDOGO MAMBO MAKUBWA.
Lamine Yamal Nasraoui (16) akiwa na mamaye wakati wa Mashindano ya Euro 2024. Lamine, winga wa Barcelona na Hispania ni miongoni mwa mawinga bora duniani. Anacheza kama mshambuliaji wa kati, mshambuliaji na winga. Baba yake alitoka Morocco, mama yake alitoka Guinea ya Ikweta.
Akiwa na umri wa miaka 16, amevunja rekodi ya Pele aliyecheza Mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 1956 alipokuwa na miaka 17.
➡️ Lamine Yamal anakuwa mchezaji mdogo aliyewahi kushinda Mchezaji Bora wa Mechi katika mchezo wa UEFA!
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kufunga kwenye Euro.
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kuasist kwenye Euro.
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kushiriki katika Euro.
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kushiriki katika el Clásico.
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kufunga katika mchezo wa La Liga.
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kuasist Barça.
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kuwa katika historia ya Barcelona kufikisha michezo 50 rasmi akiwa amevalia jezi ya Blaugrana.
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kushiriki katika mechi rasmi ya mtoano ya moja kwa moja ya UEFA Champions League.
◉ Mchezaji mdogo mchezaji aliyewahi kufunga mabao mawili katika historia ya La Liga, bila shaka akiwa amevalia jezi ya Barcelona tena.
◉ Mchezaji mdogo aliyewahi kufika kwenye jukwaa la tatu bora la Golden Boy, ambalo tayari lilikuwa limepangwa mwaka mmoja uliopita.