Aliyekuwa kocha wa Liverpool ametupilia mbali ofa ya kurejea mzigoni baada ya timu ya taifa ya Marekani kumfuata kwa ajili ya kocha mkuu mpya wa timu ya taifa hilo.
Jaribio hilo la Shirikisho la soka la Marekani kumtaka Klopp linakuka siku moja baada ya kumfuta kazi Gregg Berhalter kama kocha mkuu wa timu ya taifa hilo kufuatia mwenendo usioridhisha kwenye michuano ya Copa America 2024.
Marekani ilimaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi lao nyuma ya Uruguay na Panama na kushindwa kufuzu hatua ya robo fainali ya michuano hiyo.
Itakumbukwa Mjerumani huyo alitangaza kujiuzulu nafasi yake kama kocha mkuu wa Liverpool kwa lengo la kuchukua mapumziko ya ukocha.
Katika miaka tisa ya utumishi wake Liverpool aliiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa kwanza Ligi Kuu England baada ya takribani miongo mitatu mnamo 2020 sambamba na kutwaa klabu Bingwa Ulaya mnamo 2019.