CHADEMA Yajiweka Sawa Baada ya Peter Msigwa Kuondoka

0:00

10 / 100

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Kanda ya Nyasa kimesema kuondoka kwa aliyekuwa mgombea wa nafasi ya uenyekiti wa chama hicho na mbunge wa zamani wa Iringa Mjini Peter Msigwa hakuathiri chochote kutokana na kwamba chama hicho kuwa na jeshi kubwa la watu wenye uwezo mkubwa wa kukiongoza chama.

Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi (Sugu) amesema hayo mjini Iringa katika kikao cha baraza la mashauriano la chama hicho.

Joseph Mbilinyi amewataka wanachama na viongozi wa CHADEMA kanda hiyo kuondoa tofauti zilizojitokeza wakati wa uchaguzi na badala yake sasa waungane na kuwa kitu kimoja ili kwa pamoja washiriki katika kukijenga chama na huku akiwasihi kuwa tayari kushiriki chaguzi zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwakani.

“Tuungane ajenda ya kwenda kushinda uchaguzi na hili ni muhimu sana na ili kufanikiwa hayo yote tunahitaji nidhamu na upendo katika kusimamia yale tunayotarajia, tuwe tayari kwa chaguzi zijazo za serikali za mitaa na uchaguzi mkuu tusiache nafasi zote na tujiandae kwa nguvu zote kwa ajili ya uchaguzi wa mwakati na lengo ni kushinda majimbo angalau ishirini kati ya majimbo thelathini na moja ya kanda ya nyasa,” amesema Sugu

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CHADEMA mkoa wa Iringa William Mungai amewasihi wajumbe wa baraza hilo kwenda kuunganisha nguvu ya vijana kutokana na nafasi kubwa waliyonayo ndani ya chama.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

MFAHAMU LUISA YU BINADAMU ALIYETEMBELEA NCHI ZOTE...
MAKALA Ajuza wa miaka 73 , Luisa Yu ameweka rekodi ya...
Read more
Polisi Yapiga Marufuku Maandamano na Mikusanyiko ya...
Jeshi la Polisi limepiga marufuku maandamano na mikusanyiko ya aina...
Read more
SITI BINTI SAAD: JOHARI LA MUZIKI WA...
Siti Binti Saad (1880 - 1950), alikuwa ni mwimbaji maarufu...
Read more
MASHABIKI 11 WAJERUHIWA KWENYE MCHEZO ...
MICHEZO
See also  GIORGIA MELONI AOMBA KULIPWA FIDIA KWA KUHUSISHWA NA VIDEO ZA NGONO
Mashabiki 11 wa soka wamejeruhiwa baada ya fataki kurushwa...
Read more
SHABIKI AFIA UWANJANI
MICHEZO Mchezo wa Ligi kuu ya Uhispania (LALIGA) kati ya...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply