𝗞𝗘𝗦𝗜 𝗬𝗔 𝗠𝗔𝗚𝗢𝗠𝗔 𝗜𝗠𝗘𝗙𝗨𝗡𝗚𝗪𝗔 𝗡𝗔 𝗜𝗠𝗘𝗞𝗪𝗜𝗦𝗛𝗔

0:00

9 / 100

Rais wa Yanga Eng. Hersi Said, kamati ya Utendaji ya Yanga na Bodi ya wadhamini wanaendelea na majukumu yao yote kama kawaida kwa sababu waliingia madarakani kupitia katiba halali iiyopewa baraka na Serikali pamoja na TFF (FCC, BMT)

Young Afticans Sports Club imefungua kesi ya Jinai Kisutu dhidi ya Juma Magoma na wote waliohusika KUGHUSHI saini za wajumbe wa Bodi ya wadhamini, Mama Fatma Karume na mzee Jabil Katundu.

Pia Magoma na wenzie watapelekwa mbele ya mkutano Mkuu kama ni wanawachama halali mkutano mkuu utachukua hatua ya kuwafuta UANACHAMA kwa mujibu wa katiba ambayo inakataza masuala ya kikatiba na Migogoro yoyote yakimpira ndani ya Yanga kupelekwa mahakamani.

Yanga SC imeiaandikia barua Mahakama isongeze mbele muda wa Klabu hiyo kufanya mapitio ya kesi kwa sababu haikuwahi kushiriki kwenye kesi hiyo.

MAHAKAMA ILITOA HUKUMU BILA YA KUWEPO KWA WASHTAKIWA WHY ?!!

Kwa kuwa maombi ya mleta maombi (Juma Magoma) hayakupingwa, Mahakama ilikubaliana na nafuu zote zilizoombwa kwenye hati ya madai (PLANT).

Maana yake washitakiwa Yanga hawakushiriki katika kesi hiyo tangu ilipofunguliwa November 2022 kabla ya Hersi Said kuingia madarakani.

MSINGI WA KESI YENYEWE

6/11/2022 Magoma na Geofrey Mwipopo walifungua kesi dhidi ya Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa Yanga kwa madai kuwa hawalitambui baraza la wadhamini la Klabu hiyo wakidai liliingia kwa mujibu wa Katiba ya 2010 ambayo wanadai haijasajiliwa.

2 August 2023 Mahakama ya Kisutu ilitoa hukumu ikiwa imesikiliza upande mmoja.. hukumu hiyo haikutekelezwa na Yanga. Mei 2024 Magoma na wenzie walipeleka maombi ya kukazia hukumu kwa Hakimu Mkazi Kisutu, kuomba Mahakama kulifuta baraza la wadhamini wa Yanga na kuutoa uongozi wa Yanga na kutaka wakabidhiwe timu na Asset zote za Yanga waendeshe wao.

See also  Leicester City will be without injured forward Patson Daka for "a few months", says new manager Steve Cooper.

Wao wanaamini katiba ya mwaka 1968. Katiba iliyofanyiwa marekebisho 2011 na 2021 hawaitambui kwa hiyo mambo yote yaliyofanyika kuanzia 2010 hadi leo waaliiambia mahakama iyabatilishe, kwahiyo viongozi wote hadi makombe yote tangu 2010 ni BATILI?

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Wunmi reacts after pathologist says the cause...
CELEBRITIES The pathologist had testified that the singer’s body had...
Read more
Pep Guardiola has shocked viewers of the...
His Manchester City side had just played out a frustrating...
Read more
MWANARIADHA KIPTUM AFARIKI DUNIA ...
HABARI KUU Mwanariadha anayeshikilia rekodi ya Dunia kwenye mbio za...
Read more
Former Manchester United manager Ten Hag
Factbox on Dutchman Erik ten Hag, who was sacked as...
Read more
EDEN HAZARD ANA AKILI SANA ...
MASTORI Mwaka 2020 wakati Loic Remmy alipomzungumzia Eden Hazard; "Nilimjua Eden...
Read more

Leave a Reply