Mambo ya Ajabu ya Maisha ya Samwel Sitta na Joseph Mungai

0:00

9 / 100

Ajabu Ya Sitta Na Mungai…

  • ‘Machifu’ Wawili Walioagwa Ndani Ya Juma Moja Na Kuzikwa Kwenye Siku Moja.

Ilikuwa Novemba 2016. Samwel Sitta akiwa na umri wa miaka 74, na Joseph Mungai miaka 73. Ilikuwa zama kabla ya Uviko 19.

Sitta na Mungai walikuwa marafiki wa tangu Tabora Boys. Zama hizo shule hiyo ilikuwa moja ya shule maalum iliyotengwa na Wakoloni kwa wana wa machifu.

Hata wake zao nao walikuwa marafiki waliokutana Chuo Cha Ualimu Mpwapwa. Magreth Sitta akaja kuwa Kiongozi wa Chama cha Walimu. Hata akawa Waziri na sasa ni Mbunge.
Mary Mungai akaja kuwa Kiongozi wa Chama cha mchezo wa Netball, Chaneta na pia mmiliki wa Shule za Sekondari.

Wawili hawa, Sitta na Mungai mama zao walitokea kwenye koo kubwa za kichifu; Mama wa Samwel Sitta, Zuena Said Fundikira, ni binti wa Chifu Fundikira ambaye babu yake ni Mtemi Isike Kiyungi.

Mama wa Joseph Mungai alitokana na ukoo wa Malangalila unaotokana na Chifu Mkwawa. Hivyo, akina Malangalila na Mwamuyinga ni wajomba zake Joseph Mungai kutoka ukoo wa Kichifu wa Mkwawa.

Hivyo, wawili hawa mbali ya urafiki wao wa tangu shule uliowapelekea hadi kufanya kazi kama Mawaziri kwenye Serikali za Awamu Nne, pia walikuwa watani wa jadi. Ni kwa vile Wahehe chini ya Chifu Mkwawa walipigana vita na Wanyamwezi chini ya Mtemi Isike .

Katika namna ya kusuluhisha mgogoro, Chifu Isike alimuozesha binti yake kwa Chifu Mkwawa.

Hivyo, kikosi kidogo cha Wakonongo kilitumwa na Isike kumsindikiza binti huyo. Walipoikaribia Iringa, Mkwawa alituma watu wake kwenda kumpokea binti huyo mrembo. Ni nje kidogo ya Iringa mahali ambapo hadi hii leo panaitwa Ikonongo. Wahehe walimbatiza binti huyu kwa jina la ‘ Iyagila.’

See also  WE ARE MUCH BETTER POSITIONED FOR FUTURE SUCCESS THAN MANCHESTER UNITED

Na Wakonongo wale waliamua kuweka makazi yao hapo. Ni nje kidogo ya Manispaa ya Iringa, jirani na Chuo Kikuu cha Mkwawa.

Aidha, dalili za ujio wa Wakonongo mahali hapo ni uwepo , hadi leo, wa watu wa asili ya Kikonongo. Aidha, kuna miti mingi ya miembe waliokuja nayo Wakonongo kutoka Tabora, enzi hizo. Mwanamuziki mahiri Hamza Kalala, naye ni wa asili ya Wakonongo.

Mwezi ule wa Novemba 2016 na wiki husika, hakika ilikuwa ni ya huzuni. Ni kwa vile marafiki hawa wawili hawakuweza kuagana.

Na kwa vile, wote wawili marafiki zao wengi ni wa wote wawili, basi, ikabidi hata siku za kuwaaga Sitta na Mungai zipishane hata kwa siku moja ili marafiki wapate kuwaaga .

Wote wawili walizikwa katika siku moja ya Jumamosi, mmoja Mufindi na mwingine Urambo.

Wapumzike Kwa Amani, Chifu Sitta na Chifu Mungai.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SERIKALI YATOA MAAGIZO 18 KUIKABILI EL NINO...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo....
Read more
NI KWANINI VIJANA NCHINI JAPAN HAWAPENDI KUINGIA...
Kiwango cha uzazi nchini Japan ambacho kimezidi kushuka kwa kasi...
Read more
13 WAYS TO CORRECT YOUR WIFE WITHOUT...
LOVE TIPS ❤ 1: LOWER YOUR VOICEDon't shout at her,...
Read more
CODY GAKPO ASIMULIA FURAHA YAKE KUWA NDANI...
MICHEZO Mshambuliaji kutoka nchini Uholanzi Cody Gakpo amefichua kuwa alifanya...
Read more
HISTORIA YA VITAL KAMERHE LWA KANYIGINYI NKINGI...
NYOTA WETU Siasa ni taaluma kama itafanywa na wataalamu,siasa ni...
Read more

Leave a Reply