Mfahamu Mrithi wa Ugombea Urais wa Marekani Baada ya Joe Biden Kujiondoa?

0:00

9 / 100

Rais wa Marekani Joe Biden amesema atasimama na Makamu wake wa Rais Kamala Harris kuchaguliwa kuwa mgombea mteule wa Chama cha Demokrati katika uchaguzi wa Novemba.

Rais Biden alitangaza kumuunga mkono Kamala kupitia ukurasa wake wa X (zamani Twitter), muda mfupi baada ya kutangaza uamuzi wa kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho.

Akirejelea uamuzi wake wa “kutokubali uteuzi” na kuelekeza “nguvu” zake zote kwenye majukumu yake ya urais, Biden alisema kumchagua Harris kama Makamu wake wa Rais ndio “uamuzi bora” aliofanya.

“Leo nataka kutoa usaidizi wangu kamili na kumuidhinisha Kamala kuwa mteule wa chama chetu mwaka huu. Wanademokrasia – ni wakati wa kukusanyika na kumpiga Trump. Wacha tufanye hivi,” Biden aliandika.

Muda mfupi kabla ya kumuidhinisha Harris, Biden alitoa barua ya wazi kutangaza kujiondoa kwenye kinyang’anyiro cha urais.

“Ingawa imekuwa nia yangu ya kutaka kuchaguliwa tena, naamini ni kwa manufaa ya chama changu na nchi kwa mimi kujiuzulu na kuzingatia tu kutimiza wajibu wangu kama Rais kwa muda wote uliosalia wa muhula wangu,” aliandika. , akiahidi kulihutubia taifa kuhusu suala hilo baadaye.

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related News 📫

NAFASI YA UENEZI INAVYOITESA CCM ...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
NEEDS TO STOP THE LIES IN YOUR...
LOVE ❤ 12 NEEDS TO STOP THE LIES IN YOUR...
Read more
Paris St Germain to go to court...
Paris St Germain will take their wage dispute with Kylian...
Read more
Chelsea thump Villa 3-0 to move joint...
LONDON, - Expertly taken goals from Nicolas Jackson, captain Enzo...
Read more
See also  SAFARI YA KUMUONDOA PUTIN YAANZA NA 16

Leave a Reply