Maandamano ya Ngorongoro Yamuibua Mbowe Atema Cheche

0:00

5 / 100

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe ameitaka serikali kukaa chini na wakazi wa Ngorongoro na kuona namna ya kumaliza changamoto zilizopo eneo hilo badala ya kutumia nguvu.

Mbali na hilo, Mbowe amemtaka Rais Samia Suluhu Hassan kuwasikiliza wananchi wa Ngorongoro pamoja na kuwarejeshea huduma za kijamii.

Mbowe ameyasema hayo leo Alhamisi Agosti 22,2024 alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari makao makuu ya chama hicho, Mikocheni jijini Dar es salaam.

Kauli hiyo imekuja kutokana na maandamano yanayoendelea ya baadhi ya wakazi wa hifadhi ya Ngorongoro wanaopinga kinachotajwa kuwa ni kufutwa kwa vijiji vilivyomo ndani ya hifadhi hiyo pamoja na kuondolewa kwa huduma mbalimbali za kijamii ikiwemo huduma za kiafya, vituo vya kupigia kura na mengine.

“Kuna Genocide/Uangamizaji mkubwa unaendelea Ngorongoro,haikubaliki kuwaondolea huduma za kibinadamu Wamaasai” amesema Freeman Mbowe

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

16 ADMIRABLE ATTITUDES THAT MAN FALL IN...
LOVE ❤ If you don't want to grow white hairs...
Read more
Brad Gilbert announces end of Coaching Relationship...
World No. 6 Coco Gauff and coach Brad Gilbert are...
Read more
Guardiola said any push for a more...
The push for a more favourable match schedule must come...
Read more
MZEE RUKHSA AMEONDOKA BILA DENI
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
RAIS WA GUINEA BISSAU KUZURU TANZANIA KIKAZI
HABARI KUU Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe....
Read more
See also  TFF YAMFUTA KAZI AMROUCHE HUKU CAF IKIMFUNGIA

Leave a Reply