KIFAFA CHA MIMBA NI NINI?

0:00

10 / 100

Kifafa cha mimba ni ugonjwa unaowapata wanawake wajawazito, hasa wenye mimba za kwanza.

Kwa walio wengi, ugonjwa huu hutokana na kupanda kwa msukumo wa damu (High blood pressure). Ugonjwa huu utokeapo, mgonjwa hupatwa na degedege (convulsion).
Ugonjwa huu unajulikana kwa kitaalamu kama Eclampsia.

Kifafa cha uzazi au wengine wanakiita kifafa cha mimba ni miongoni mwa matatizo yanayosababisha vifo vya wajawazito nchini.

Kifafa cha mimba kinaweza kutokea wakati wa ujauzito, wakati wa kujifungua au baada ya kujifungua.

Sababu la tatizo hili bado wataalamu wa tiba duniani hawajagundua, Ila kuna baadhi sababu zinahisiwa kusababisha tatizo hili ambazo ni pamoja na:

1) Mimba ya kwanza, hususani katika umri mdogo chini ya miaka 20 na mimba za uzeeni baada ya miaka 35.

2) Ugonjwa wa shinikizo la damu au kisukari kabla ya kubeba mimba.

3) Wanawake wenye wenza wengi (multiple sexual partners) wapo katika hatari ya kupata kifafa cha mimba.

4) Wanawake ambao wazazi, au ndugu zao wa karibu waliwahi kupatwa na matatizo ya kifafa katika mimba zao.

5) Wanawake waliopatwa na kifafa cha mimba zao za kwanza wapo katika hatari ya kupata kifafa hicho tena katika mimba zinazofuata.

6) Wanawake wenye mimba ya mapacha wapo katika hatari zaidi ya kupata kifafa cha mimba kuliko mimba ya mtoto mmoja.

7) Ugonjwa wa figo kwa mama mjamzito.

DALILI ZA KIFAFA CHA MIMBA:

Kwa sababu shinikizo kubwa la damu kwa mjamzito (pre eclampsia) ndio chanzo kikubwa cha kifafa cha mimba.

Mjamzito anaweza kuwa na dalili za changamoto zote mbili, yaani akawa na dalili za kuongezeka zaidi kwa presha ya damu (high blood pressure), kuvimba miguu na mikono.

See also  DEREVA WA SHULE YA MEMORIAL ASOMEWA MASHTAKA

Dalili kuu za kifafa cha mimba ni pamoja kupoteza fahamu, degedege (convulsion) inayo ambatana na uwepo wa protini kwenye mkojo (proteinuria).

Dalili zingine ni kama ifuatavyo:

1) kuongezeka uzito kupita kiasi.

2) kichefuchefu na kutapika kupita kiasi.

3) Kupata shida wakati wa kukojoa (dysuria).

4) Maumivu makali ya kichwa (severe headache).

5) kuvimba uso na vidole.

6) Kuona giza au kutoona vizuri (blurred vision).

Kumbuka: Mara nyingi kifafa cha mimba hutokea kwa mimba yenye umri wa wiki 20 na zaidi, na inaweza itokee wakati wa ujauzito au mara tu baada ya kujifungua.

🍂Kifafa cha mimba ni ugonjwa wa dharura (medical emergency condition), hivyo madaktari na manesi watakusanyika kwa pamoja kumhudumia mgonjwa.

Baada  ya  degedege kuisha na kupatiwa dawa za presha, mama ataanzishiwa dawa za uchungu (oxytocics) hata kama mimba ilikuwa bado haijafikia umri wa kujifungua, kwa kuwa kuna ulazima wa kuokoa maisha ya mama kwanza (mother’s life first) mama anaweza pia kujifungua  kwa kufanyiwa upasuaji kama patakua na uhitaji wa kufanya hivyo.

Yafuatayo ni madhara yanayoweza kutokea endapo mama mjamzito mwenye kifafa cha mimba atashindwa kupata matibabu haraka ambayo ni pamoja na:

1) Wakati wa kifafa cha mimba kuna uwezekano mkubwa zaidi wa kondo la nyuma (placenta) kubanduka na kutoka kwenye mfuko wa uzazi, hali hii kwa kitalaamu hujulikana kama placental abruption ambapo mwanamke mwenye tatizo hili hutokwa damu nyingi zaidi na hata kupelekea kifo.

2) Uwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa njiti na matatizo yanayoambatana na hali hiyo huongezeka.

3) Mgonjwa anaweza kupata tatizo la damu kushindwa kuganda linaloitwa disseminated intravascular coagulation  (DIC). Tatizo hili linaweza kusababisha mama kuvuja damu nyingi na hata kufa.

See also  7 BODY PARTS YOU SHOULD NEVER IGNORE DURING FOREPLAY.

Mama mjamzito anashauriwa kufanya mambo yafuatayo ili kuepuka kupata kifafa cha mimba ambayo ni pamoja na:

1) Ni muhimu kwa wanawake wote wajawazito kupata huduma za matibabu mapema na kwa mwendelezo. Hii itasaidia utambuzi wa mapema na matibabu kwa viashiria vya kifafa cha mimba kabla tatizo halijawa kubwa zaidi.

2) Kutibu viashiria (preeclampsia) kunaweza kuzuia tatizo hili.

Kama ilivyoandikwa hapo juu, kifafa cha mimba ni ugonjwa wa dharura (medical emergency condition), hivyo basi mama mjamzito mwenye tatizo hili analazimika kuwaishwa haraka hospitali ili kunusuru afya yake na mtoto aliye tumboni.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Senate postponed its resumption date session from...
In a significant update from the Senate, the resumption date...
Read more
SABABU DANI ALVES KUACHIWA HURU
MICHEZO Mahakama ya Hispania imesema mlinzi wa zamani wa FC...
Read more
SITI BINTI SAAD: JOHARI LA MUZIKI WA...
Siti Binti Saad (1880 - 1950), alikuwa ni mwimbaji maarufu...
Read more
MUME WA RIHANNA AFUNGUKA JUU YA MKE...
NYOTA WETU. ASAP ROCKY hakuacha tabasamu lake lififie alipokuwa akijadili...
Read more
Northeastern Elders Laud Duale's Reappointment as Defense...
Community Elders in Garissa County have welcomed the reappointment of...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply