Mahakama kuu imesitisha azimio la Bunge la seneti la kuunga mkono ombi la kuondolewa kwa aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua lililowasilishwa kwenye Bunge hilo Alhamisi, Oktoba 17.
Katika uamuzi huo uliotolewa leo Ijumaa 18/10/ 2024 na Jaji Chacha Mwita umetaja ombi la Gachagua limeibua masuala muhimu ya kisheria na maslahi ya umma, hivyo ametoa amri ya kusitisha utekelezwaji wa kuteuliwa kwa mbadala wake hadi Oktoba 24, 2024 kesi hiyo itakapotajwa mahakamani.
Uamuzi huo umekuja masaa machache baada ya Bunge la Kitaifa la Kenya kuidhinisha uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kama Naibu Rais wa Kenya, uteuzi wa Kindiki uliungwa mkono na wabunge 236 waliopiga kura ya ndio.
Gachagua kupitia kwa wakili wake Mkuu Paul Muite, alidai kuwa mchakato wa kumbandua mamlakani ulikuwa na kasoro na haukuwa na ushahidi wa kutosha.
Rais Ruto sasa atakabiliwa na wakati mgumu, iwapo mahakama haitomtia hatiani Rigadhi Gachagua.
Wakati wa kampeni ya Ruto katika uchaguzi Mkuu wa 2022, Rais Ruto alisema hatoruhusu Naibu wake kuteswa na kudharauliwa na watumishi wa chini kama alivyofanyiwa yeye na Bosi wake Uhuru Kenyatta.
GACHAGUA APINGA KUBANDULIWA OFISINI.
Aliyekuwa Naibu Rais wa Kenya Rigathi Gachagua amepeleka kesi mahakamani kupinga mchakato wa Kubanduliwa kwake madarakani kama Naibu Rais wa Kenya.
Baada ya seneti kupitisha hoja ya kumwondoa, Gachagua amedai kuwa hakupata nafasi ya kujitetea ipasavyo kwani alikosa kuhudhuria kutokana na kuugua ghafla.
Timu yake ya mawakili, inayoongozwa na Wakili Mkuu Paul Muite, inadai kuwa mchakato wa kumbandua ulikuwa na kasoro na haukuwa na ushahidi wa kutosha. Wanaitaka mahakama kusimamisha uteuzi wa Profesa Kithure Kindiki kama Naibu Rais mpya hadi kesi yao itakaposikilizwa.
Wakati wa utawala wake,Gachagua alikuwa akifika ofisini saa 11 alfajiri na kuwa kiongozi wa Juu aliyekuwa anawai ofisini.
Wadadisi wa masuala ya kisiasa wanasema uamuzi wa bunge la seneti Kumbandua Gachagua mamlakani haufai kusherehekewa na walio mamlakani kwani huenda mbanduo huo ukawakumba na wao kwa siku za usoni.