TUNDU LISSU akerwa na uhusiano wa Mbowe na Serikali

0:00

4 / 100

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Tundu Lissu , ameweka wazi sababu za kuwania nafasi ya uenyekiti wa chama hicho ngazi ya taifa na kutoa maoni yake kuhusu changamoto za kisiasa nchini.

Lissu ameyasema hayo wakati wa mahojiano ya hivi karibuni na kituo cha habari cha Voice of America (VOA), ambapo amezungumzia masuala ya mabadiliko ndani ya chama na hatua za kulazimisha mageuzi ya kidemokrasia nchini.

Lissu amesema CHADEMA inahitaji uongozi mpya ambao utaiondoa nchi kutoka kwenye mkwamo wa kisiasa uliopo sasa. Ameeleza kuwa mazungumzo ya maridhiano na Rais Samia Suluhu Hassan ambayo yamefanyika kwa takriban miaka miwili hayajazaa matunda yoyote, akisisitiza kuwa ni wakati wa kuanzisha “Nguvu ya Umma” (mass mobilization) ili kuamsha taifa na kushirikiana na asasi za kiraia na vyama vingine vya siasa kulazimisha mabadiliko ya kidemokrasia.

“Tunatakiwa kufanikisha mabadiliko makubwa ya kidemokrasia ili kulazimisha mabadiliko ya mfumo wa uongozi,” amesema Lissu.

Alipoulizwa kuhusu tofauti kati yake na Mwenyekiti wa sasa wa CHADEMA, Freeman Mbowe , Lissu amekiri kuwa kuna tofauti za kimsingi juu ya namna ya kukipeleka chama mbele. Amedai kuwa uongozi wa sasa haujachukua hatua za kutosha kupambana na changamoto zinazolikabili taifa, kama vile utekaji na mauaji ya wanachama wa chama hicho.

“Chama kinaonekana kipo nusu kaputi kwa sababu Mwenyekiti haonekani kutaka kubomoa daraja na uongozi wa Rais Samia,” amesema Lissu.

Lissu ameeleza msimamo wa CHADEMA kuhusu kushiriki uchaguzi, akisema chama hicho hakitashiriki chaguzi zozote zijazo kama hakutakuwa na mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi. Amerejelea uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, na mitaa uliofanyika hivi karibuni, akisema ulikuwa “majanga” kwa kiwango cha udanganyifu kilichofanywa.

See also  Davido stirs uproar as he throws hot shade at Wizkid

“Tumesimama kwenye msimamo wa No Reforms, No Election. Lazima tupiganie mabadiliko kabla ya kushiriki chaguzi,” amesisitiza Lissu.

Lissu ametoa wito wa mabadiliko ndani ya CHADEMA, akisema chama hicho hakiwezi kupambana na changamoto za nje kama hakitasafisha mfumo wake wa ndani. Amependekeza kuwepo kwa ukomo wa uongozi na kuweka mifumo inayohakikisha uwazi na uwajibikaji ndani ya chama.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Utambulisho wa Kylian Mbappe Kufuru Tupu
Klabu la Real Madrid ya nchini Hispania, imetangaza kuuzwa kwa...
Read more
Messi hits hat-trick as Argentina hammer Bolivia...
BUENOS AIRES, - Lionel Messi scored his 10th international hat-trick...
Read more
Tragic Road Accident in Garissa Leaves 10...
A road accident in the Katumba area along the Garissa-Nairobi...
Read more
MARRIED WOMEN MUST NOT DO WITH OTHER...
LOVE ❤ 21 THINGS MARRIED WOMEN MUST NOT DO WITH...
Read more
HATARI WANAWAKE WANAOTUMIA FRAGYL KUKOSA UJAUZITO ...
Magazeti Hujambo Mtanzania popote pale ulipo, karibu kwenye kurasa za...
Read more

Leave a Reply