SABABU ZA KLABU YA YOUNG AFRICANS KUFUNGIWA KUSAJILI NA FIFA

0:00

MICHEZO

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetoa taarifa kuwa Klabu ya Young Africans (Yanga) inayoshiriki Ligi Kuu ya NBC imefungiwa kufanya usajili kwa kukiuka kanuni za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

Taarifa imeeleza kuwa uamuzi huo umefanywa na FIFA baada ya klabu hiyo kukiuka Annexe 3 ya Kanuni ya Uhamisho wa Wachezaji (RSTP) ya Shirikisho hilo.

Aidha Yanga haikuingiza uthibitisho wa malipo ya uhamisho wa mchezaji husika (jina halijatajwa) katika Mfumo wa Usajili (TMS), licha ya kukumbushwa kufanya hivyo.

Yanga imetakiwa kutekeleza matakwa hayo ya kikanuni, na kuwasilisha taarifa kwa Sekretarieti ya
Kamati ya Nidhamu ya FIFA ambapo suala hilo limefikishwa kwa ajili ya hatua zaidi.

Kutokana na uamuzi huo wa FIFA, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) nalo limeifungia klabu hiyo kufanya usajili kwa wachezaji wa ndani.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Saliba sent off as Arsenal slump to...
A brilliantly-worked goal by Ryan Christie and a Justin Kluivert...
Read more
BARCELONA YAMUONDOA DANI ALVES KWENYE ORODHA YA...
MICHEZO Klabu ya Barcelona imemuondoa Dani Alves kwenye orodha ya...
Read more
XABI ALONSO ATOA ONYO KWA WACHEZAJI WA...
MICHEZO Vinara wa Bundesliga, Bayer Leverkusen wanakaribia kupata taji lao...
Read more
KIFAHAMU KIFAA KIITWACHO SARCOPHAGUS CHA KUJIUA...
MAKALA Inaitwa "Sarco", kifupi cha sarcophagus, ni mashine iliyochapishwa kwa...
Read more
BONDIA WA KWANZA WA TANZANIA AONDOLEWA KWENYE...
MICHEZO Ajali ya kuvunjika mkono katika raundi ya mwisho ya...
Read more

Leave a Reply