CHELSEA YAACHANA NA MAURICIO POCHETTINO

0:00

MICHEZO

Uongozi wa Klabu ya Chelsea umetangaza kuachana na Kocha Mauricio Roberto Pochettino Trossero kwa makubaliano ya pande zote mbili ya kuvunja Mkataba ambao ulisainiwa mapema msimu wa 2023/24.

Kocha huyo alisaini mkataba wa miaka miwili, hivyo sehemu ya mwaka mmoja katika Mkataba wake ndio imevunjwa kwa makubaliano maalum yaliyofikia kati yake na Uongozi wa juu wa Chelsea.

Akizungumzia kuhusu kuondoka katika klabu hiyo, Pochettino amesema:

“Sina budi kuushukuru Uongozi wa Chelsea kwa nafasi kubwa waliyonipa, nimekuwa sehemu ya historia ya Klabu hii,”

“Pia ninawashukuru sana Wachezaji wangu na Mashabiki ambao siku zote tulikuwa pamoja katika kipindi cha Raha na Simanzi, ninaitakia kila la kheri Chelsea katika mpango wake mpya.”

“Ninajivunia kuiacha klabu katika nafasi nzuri, Msimu ujao itashiriki Michuano ya Ulaya, hii imetokana na kazi kubwa niliyoifanya kwa kushirikiana na Wachezaji wangu hadi siku ya mwisho ya msimu, ninawapongeza sana kwa hilo.”

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Meru Governor Faces Third Impeachment Bid over...
The Meru County Assembly has tabled a notice of motion...
Read more
MJANE WA NYAMA YA SWALA ASIMULIA SIKU...
MAGAZETI Karibu Mtanzania popote pale ulipo kwenye asubuhi ya leo...
Read more
ASLAY JINSI ALIVYOGEUKA IFTAR USIKU WA JANA...
NYOTA WETU Dunia imebadilika sana, wakati Mange Kimambi anatangaza kuja...
Read more
Kenyan Teachers' Unions Threaten Nationwide Strike Over...
The Kenya National Union of Teachers (KNUT) and the Kenya...
Read more
CRISTIANO RONALDO ASHUHUDIA PAMBANO LA FURRY NA...
MICHEZO Kiungo mshambuliaji wa Al Nassr ya Saudia Arabia, Cristiano...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  VAN GAAL AIBUA SIRI NZITO KWENYE KOMBE LA DUNIA

Leave a Reply