SABABU ZA JESHI KUONGEZA MUDA WA UTAWALA BURKINA FASO

0:00

4 / 100

Utawala wa Kijeshi wa Kapteni Ibrahim Traoré, ambaye aliingia Madarakani Septemba 2022 kupitia Mapinduzi ya Kijeshi, atarefusha kipindi chake cha uongozi wa nchi kwa miaka mitano zaidi, kulingana na katiba iliyopitishwa Jumamosi na washiriki katika mikutano ya Kitaifa huko Ouagadougou.

“Muda wa mpito umewekwa kuwa miezi 60 kutoka Julai 2, 2024,” alisema Kanali Moussa Diallo, Rais wa Kamati ya maandalizi ya mikutano .

Rais Traoré pia ataweza kusimama katika chaguzi za Urais Ubunge na Manispaa ambao utaandaliwa ili kukomesha mpito”, aliendelea kusema Kanali Diallo.

Mikutano hiyo ya kitaifa, iliyopangwa kumalizika Jumapili, ilileta pamoja wawakilishi wa mashirika ya kiraia, vikosi vya ulinzi na usalama na hata manaibu kutoka bunge la mpito siku ya Jumamosi. Vyama vingi vya kisiasa vilisusia hafla hiyo.

Utawala wa mpito ulipaswa kumalizika Julai 1, 2024, lakini mara kadhaa Kapteni Traoré alizungumzia ugumu wa kufanya uchaguzi kutokana na mazingira ya usalama nchini.

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

SABABU ILIOFANYA YANGA KUFUNGIWA HII HAPA
Dar es salaam. Klabu ya #Yanga imefungiwa kusajili baada ya...
Read more
MFAHAMU MKE WA RAIS WA AFRIKA KUSINI...
Jana, Rais Cyril Ramaphosa aliapishwa kuendelea kuongoza Taifa la Afrika...
Read more
ROBERTINHO AIKAANGA SIMBA ...
MICHEZO Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba SC. Robertinho amekosoa usajili...
Read more
Labour Union has strongly urged pres. Bola...
NLC and TUC are urging President Bola Tinubu to refrain...
Read more
PAUL MAKONDA MKUU WA MKOA ARUSHA
HABARI KUU Rais Samia Suluhu Hassan amemteua aliyekuwa Katibu wa...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

See also  TANZANIA NA WENZAKE KUANDAA AFRICON

Leave a Reply