Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kanda ya Nyasa ambaye pia anagombea kutetea nafasi hiyo katika uchaguzi wa ndani wa chama hicho, Mchungaji Peter Msigwa amewasilisha malalamiko dhidi ya Mjumbe wa Sekretarieti ya chama hicho John Mrema kwa kile alichokitaja kuwa mgongano wa masilahi katika uchaguzi wa kanda wa chama.

0:00

4 / 100

Katika barua aliyomwandikia Katibu Mkuu wa CHADEMA John Mnyika, Msigwa ameeleza kuwa mwenendo wa John Mrema unazua maswali kwani ameonesha dhahiri kuegemea upande wa mgombea mwenza wa uenyekiti wa kanda ya Nyasa Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na kuonesha dalili zote za rushwa kinyume na “Kanuni ya 1 (vi) ya Mwongozo wa Chama dhidi ya Rushwa Kwenye Uchaguzi ndani ya Chama Toleo la 2012”.

“Tarehe 24 Mei, 2024 kabla na baada ya uchaguzi wa chama wa Mkoa wa Iringa, kuanzia majira ya asubuhi lakini pia saa kumi na mbili jioni alikutana na mgombea mwenzangu wa Kanda ya Nyasa katika nafasi ya uenyekiti Mhe. Joseph Mbilinyi, Twiga Night Club ambapo mgombea mwenzangu aliweza kununua kreti 4 za bia wakaendelea kunywa na msimamizi huyu wa uchaguzi mpaka majira ya saa sita usiku” Imeeleza barua ya Msigwa.

Ameendelea kueleza kwamba kwa nyakati tofautitofauti, Mrema amekuwa akiwapigia simu wajumbe (Wapiga kura) katika ngazi ya kanda akiwashawishi wasimchague Msigwa bali wamchague Sugu kwa madai kuwa kuwa hayo ni maagizo ya Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe.

Aidha Msigwa amemtuhumu Mrema kumsaidia mgombea uenyekiti wa Baraza la Vijana CHADEMA (BAVICHA) kanda ya Nyasa Vitusi Nkuna kwa kueleza kuwa tarehe 26 Mei, 2024 Mrema ambaye pia ni msimamizi wa uchaguzi, alipanda gari ya Nkuna kutoka Iringa mpaka Makambako na kwamba siku mbili nyuma alikunywa naye pombe mpaka usiku wa manane.

Kutokana na mambo hayo, Msigwa ameomba Mrema aondolewe kwenye shughuli zinazohusiana na usimamizi wa uchaguzi na waletwe wasimamizi wengine ambao hawana masilahi binafsi katika uchaguzi huo ili haki iweze kutendeka kwa wagombea wote bila ubaguzi wala upendeleo.

Mujuni Henry
See also  "KUKOPA NI AFYA KWA UCHUMI " GEORGE SIMBACHAWENE
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Chelsea yamfukuza Mauricio Pochettino
Klabu ya Chelsea imethibitisha kuachana na kocha wake, Mauricio Pochettino...
Read more
CCM YAMPIGA CHINI DANIEL CHONGOLO ...
HABARI KUU Taarifa zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii kutokea tarehe...
Read more
MFAHAMU MISS WORLD KRYSTYNA PYSZKO
NYOTA WETU Miss Czech Krystyna Pyszko ametangazwa kuwa mshindi wa...
Read more
ANTHONY JOSHUA ATAMBA KUMPIGA FRANCIS NGANNOU KWA...
MICHEZO Bondia Anthony Joshua ametamba kumpiga mpinzani wake Francis Ngannou...
Read more
HUYU NDIYE MRITHI WA HENOCK INONGA AJAYE...
MICHEZO Mlinzi wa Klabu ya ASEC Mimosas, Anthony Tra...
Read more

Discover more from JUNIITV.ONLINE

Subscribe to get the latest posts sent to your email.

Leave a Reply