Hayo yamebainishwa na Jopo la wajumbe wa mahakama mjini New York,siku ya jana Alhamisi ambapo walisema kuwa Donald Trump anakabiliwa na mashtaka 34 ikiwemo ya kugushi hati zake za biashara.
Jopo hilo lenye wajumbe 12 lilitathmini na kutafakari kwa siku mbili ushahidi wote liliopokea na kutoa uamuzi dhidi ya Trump mwenye umri wa miaka 77 , katika kesi ya kwanza ya uhalifu dhidi ya rais wa zamani wa Marekani.
Wakili wa Trump,Todd Blance aliomba uamuzi huo wa kupatikana na hatia ubatilishwe, lakini hakimu wa Mahakama Kuu ya New York Joan Merchan alipinga hoja hiyo.
Trump alipatikana na hatia kutokana na mashtaka ya kumlipa Stormy Daniels ambaye ni mwanamke muigizaji wa filamu za ngono karibu dola 130, 000 ili kumnyamazisha, yaani “hush money” kabla ya uchaguzi mkuu wa 2016.
Hukumu ya Trump imepangwa kutolewa Julai 11, kati kati ya kampeni yake ya kujaribu kurudi kwenye White House, siku chache kabla ya kuanza kwa Kongamano la Kitaifa la chama cha Republican hapo Julai 15.
Trump bado anatarajiwa kugombania kiti cha rais wakati wa uchaguzi wa mwezi Novemba dhidi ya Rais Joe Biden aliyemshinda wakati wa uchaguzi wa 2020.
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.