NI KWANINI VIJANA NCHINI JAPAN HAWAPENDI KUINGIA KWENYE MAHUSIANO?

0:00

9 / 100

Kiwango cha uzazi nchini Japan ambacho kimezidi kushuka kwa kasi kwa miaka mingi na kufikia rekodi nyingine ya chini zaidi hivi karibuni, kimeifanya Serikali ya Nchi hiyo kuongeza ubunifu kwenye kampeni zake za kuwahimiza Vijana kuoa na kuanzisha familia ambapo sasa imezindua Program ya simu ambayo kazi yake mahususi ni kurahisisha Watu kuchumbiana.

Kwenye program hiyo na tovuti yake, Watumiaji lazima wawe hawana wapenzi wakiwa na umri zaidi ya miaka 18 na wawe wenye hamu ya kuoa na kuolewa pia wawe wanaishi au kufanya kazi katika Jiji la Tokyo ambapo Watumiaji wataombwa kuweka sifa ambazo wanatamani kuzikuta kwa wenza wao wa maisha.

Ndani ya Program hiyo yenye mambo mbalimbali, pia inaorodhesha hatua nyingine za Serikali kusaidia Wanandoa kama vile kutoa taarifa kuhusu kazi na maisha ya ndoa, malezi ya Watoto, kutoa msaada wa Makazi, kuwafundisha Wanaume jinsi ya kushiriki kwenye kazi na majukumu ya nyumbani, kulea Watoto na kutoa ushauri wa ajira na kazi.

Ukiachia mbali viwango vya kuzaliana kushuka Nchini Japan, pia viwango vya Wanandoa kupeana talaka vimeongezeka na kuongeza wasiwasi kwa Serikali ya Nchi hiyo.

Majaribio ya program hiyo yamevutia wengi akiwemo Tajiri wa dunia Mmiliki wa mtandao wa X pamoja na magari ya umeme ya Tesla Elon Musk ambaye aliandika yafuatayo kwenye X

“Nina furaha Serikali ya Japan inatambua umuhimu wa jambo hili, endapo hatua kali hazitochukuliwa, Japan pamoja na Nchi nyingine nyingi zitatoweka”

Loading

Mujuni Henry
Author: Mujuni Henry

JUNIITV

Related Posts 📫

Kiongozi wa upinzani Nchini Israel Yair Lapid...
Lapid ametoa pendekezo la kuiunga mkono serikali iwapo washirika wa...
Read more
BIG SECRETS IN MARRIAGE
Secret...
Read more
SABABU YA VITA YA BARAKA MPENJA NA...
MASTORI
See also  Yul Edochie speaks out again, throws shade at critics after dragging later Junior Pope
"..Alikuja Mwamba wa Umarila Baraka Mpenja "sauti ya Radi"...
Read more
I regret opening up about my sexuality...
American singer, Billie Eilish has said she regretted making her...
Read more
Man United edge past Bodo/Glimt to give...
MANCHESTER, England, 🏴󠁧󠁢󠁥󠁮󠁧󠁿 - Manchester United came from behind to...
Read more

Leave a Reply