Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema kanuni zake za sasa ni rafiki zaidi ikilinganishwa na namna ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita katika vigezo vya utoaji na ufungiaji leseni za uchapishaji maudhui katika chaneli ya YouTube hali inayochochea muktadha wa maudhui ya kitanzania na sekta ya ubunifu.
Afisa Tehama Mwandamizi wa TCRA, Brian Kalinga ameyasema hayo leo Juni 10, 2024 wakati akizungumza na Daily News Digital kwenye Maonesho ya 48 ya Biashara ya Kimataifa maarufu ‘sabasaba’ yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Nyerere, Barabara ya Kilwa jijini Dar es salaam.
Amesema habari njema ni kwamba, awali gharama ya leseni ili kuhalalisha umiliki wa chaneli ya YouTube ilikuwa ni Sh 1,100,000 lakini sasa hivi unalipia nusu ya fedha hizo kwa leseni ya kipindi cha miaka mitatu.
Ameongeza kuwa suala la mapinduzi na mifumo ya mitandao ya kijamii imebadilisha taswira ya habari na vyombo vya habari ‘mainstream media’ vinavyotakiwa kuendeshwa na hata kuteteresha mapato yake.
Kutokana na hilo, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliunda kamati ya kutathmini hali ya sekta ya habari ili kuangalia namna gani teknolojia inavyopaswa kutumika ili kila upande unufaike.
“Tuliwaalika wataalamu kutoka UK (Uingereza) kwaajili ya kubadilishana uzoefu na kutushauri namna bora ya kufanya kazi yenye tija na bila kuathiri upande wowote.” Ameeleza.
–
Related Posts 📫
Discover more from JUNIITV.ONLINE
Subscribe to get the latest posts sent to your email.